• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Staff Mail |
    • Malalamiko |
Tanga City Council
Tanga City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Tanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Usafi wa Mazingira
      • Mipangomiji na Maliasili
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jiamii na Vijana
      • Maji
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Manunuzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
    • Kata
    • Mitaa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Utalii
    • Sekta ya Madini
    • Sekta ya Elimu
    • Sekta ya Viwanda
    • Maeneo ya Nyumba na Makazi
    • Sekta ya Misitu na Mashamba ya Miti
    • Sekta ya Uvuvi
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Usafi na Mazingira
    • Maji
    • Ardhi na Maliasili
    • Ujenzi na Miundombinu
    • Uwezeshaji Wananchi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi, Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango Miji na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Siku za Kumuona Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi Iliyoidhinishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Kanuni
    • Fomu Mbalimbali
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Majarida
    • Taarifa za Miradi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
  • TangaTV

UWANJA WA NANE NANE MOROGORO KUGEUZWA DARASA.

Imewekwa: July 16th, 2022

UWANJA WA NANE NANE MOROGORO KUGEUZWA DARASA.

Watoto kupata elimu bure.

      Mussa Labani - Morogoro

Zikiwa zimebaki wiki mbili kuanza kwa maonyesho ya kilimo, mifugo na uvuvi, maarufu kama maonyesho ya nane nane, hapo Augosti 1, 2022, maandalizi kwa kanda ya mashariki inayojumuisha mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani na Morogoro yamepamba moto huku zikitarajiwa teknolojia mbalimbali za kisasa kufundishwa uwanjani hapo na kuufanya uwanja wa Mwalimu J. K. Nyerere uliopo Manispaa ya Morogoro kugeuka kuwa darasa la uboreshaji kilimo, mifugo na uvuvi.

Akizungumza wakati wa kikao cha pili cha Kamati Kuu ya mandalizi ya maonyesho hayo, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Adam Malima ambaye ndiye aliyeongeza kikao hicho, amesema lengo kubwa la maonyesho hayo ni kuhakikisha kwamba wananchi wanaokuja kwenye maonyesho wanatoka na mbinu bora kwenda kuzalisha kwenye mashamba yao.

“Tunataka watu waje wajiulize. Kama linawezekana hapa, linawezekana shambani kwangu. Kwa hiyo akija atakutana na wenyeji wake (katika banda au vipando) atauliza maswali, tunataka kila kinachoonekana hapa kiweza kutafsirika na kupelekwa kwenye mashamba ya wakulima huko kwenye maeneo yao” amesema Malima.


Aidha Kamati Kuu imeamua kufuta kiingilio cha shilling Mia Tano (500) kinachotozwa kwa watoto, na hivyo kwa kuanzia maonyesho ya mwaka huu, watoto wataingia bure na kuweza kupata elimu kwa kuona kwa vitendo tofauti na shuleni ambako ni nadharia pekee.

Katika kuboresha teknolojia za kilimo, mifugo na uvuvi, Halmashauri zinazounda kanda ya Mashariki (kutoka Mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani na Morogoro) na wadau wamehamasishwa na Kamati Kuu kuandaa vipando vinavyoweza kuchukua muda mfupi ili wananchi waweze kujifunza.


Wameshauriwa pia kutoa elimu ya namna bora ya uaandaji wa mashamba, upandaji, uvunaji na uhifadhi wa mazao. Kwa upande wa mifugo, Halmashauri na wadau wanashauriwa kuonesha teknolojia zinazohusiana na uongezaji wa tija katika uzalishaji kwenye mifugo, huku ukitolewa mfano  wa uhimilishaji, uzalishaji na uhifadhi wa malisho kwa kutumia teknolojia rahisi kama vile mashine za kuchanganyia chakula.


Katika maonyesho hayo ambayo yamezidi kuvutia washiriki wa ndani ya nje, katika sekta ya uvuvi, Kamati Kuu imewataka waoneshaji kuonyesha mbinu rahisi za kuongeza tija katika uzalishaji wa samaki kama utengenezaji wa chakula bora, uzalishaji wa vifaranga bora vya samaki na uoneshaji wa zana sahihi zinazotumika katika uvuvi, kilimo cha mwani, unenepeshaji wa majongoo bahari na kaa.

Kikao cha Kamati Kuu ya maandalizi ya maonyesho ya kilimo, mifugo na uvuvi – Nane nane kwa Kanda ya Mashariki, kimefanyika katika ukumbi uliopo katika banda la maonyesho la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ndani ya uwanja wa maonyesho wa nane nane Manispaa ya Morogoro kikitanguliwa na Kikao cha Kamati ya Wataalamu kilichokaa siku moja kabla, na wajumbe wa Kamati Kuu wakiwa ni Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, pamoja na wataalamu wao kutoka Sekretarieti za Mikoa, Wakuu wa Sehemu za Mifugo na Kilimo pamoja na Maafisa Mawasiliano Serikalini kutoka mikoa inayounda kanda ya maonyesho.

Maonesho ya mwaka huu, yanafanyika baada ya kusitishwa mwaka 2021 na kisha kurejeshwa tena mwaka huu 2022. Kauli Mbiu ya Maonesho ya Nane Nane mwaka 2022 ni “Ajenda 10/30: Kilimo  ni Biashara, Shiriki Kuhesabiwa kwa Mipango Bora wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi”


Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ. March 09, 2025
  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA JIJI TANGA September 27, 2024
  • TAARIFA YA MSIBA September 18, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 26, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • TANGA: MABORESHO DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KUANZA FEB. 13, 2025

    February 04, 2025
  • MENEJIMENTI WAPONGEZWA UTEKELEZAJI MIRADI, UMALIZIAJI WA VIPORO.

    February 04, 2025
  • AFUA ZA LISHE ZAFANYA VIZURI TANGA JIJI

    January 24, 2025
  • KAMATI YA FEDHA NA UONGOZI YAKAGUA MIRADI.

    January 16, 2025
  • Angalia Zote

Video

Baraza la Madiwani la kwanza 2020
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matumizi ya TEHAMA kwa Jiji la Tanga
  • Kata na Mitaa ya Jiji la Tanga
  • Manual ya mfumo wa FFARS
  • Muongozo wa ugawaji wa kitambulisho cha mjasiliamali
  • Jarida la Mifumo Yetu - Novemba 2018-Januari 2019
  • Kupata leseni ya Biashara
  • Tangazo kuhusu watumishi waliomba vibali vya uhamisho
  • Kuanza Ujenzi na Kupata Kibali cha Ujenzi
  • Kuhusu kupata kibali cha kusafiri nje ya nchi

Tovuti Linganifu

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Mfumo wa Kuomba Vibali vya Nje ya Nchi
  • Facebook
  • Twitter
  • Instagram
  • Tanzania Government Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Independent Avenue

    Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga

    Simu ya Mezani: 027 2643068

    Simu ya Mkononi:

    Baruapepe: info@tangacc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.