Julai 11, 2024.
Timu ya wataalam kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na chuo cha Mipango Mwanza na Chuo Kikuu cha Dar es salaam pamoja na wataalam kutoka ofisi ya Halmashauri ya Jiji la Tanga, na Wizara ya Mifugo na Uvuvi wamefanya ziara katika vikundi vinavyofanya shughuli za uchumi wa buluu, katika Jiji la Tanga, ikiwa ni maandalizi ya ujio wa mradi wa "Bahari Maisha" chini ya ufadhili wa UNDP, wenye lengo la kuongeza thamani kwenye mazao ya bahari.
Vikundi vilivyotembelewa ni pamoja na vikundi vya kilimo cha mwani pamoja na unenepeshaji wa kaa. Ambapo timu hiyo ya wataalam ilikutana na umoja wa wakulima wa mwani Sahare Kijijini wenye jumla ya vikundi 29 pamoja na kikundi cha Chimbachi kinachofanya shughuli za Unenepeshaji kaa katika mtaa wa machui.
Timu hiyo pia ilitembelea kituo cha uzalishaji samaki kilichopo chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
Mradi wa Bahari Maisha unakusudiwa kutekelezwa katika Jiji la Tanga kwa kuviwezesha vikundi vya wakulima wa mwani, wafugaji wa jongoo bahari, kaa, na mazao mengine ya bahari na udhibiti wa taka/masali kutoka kwa mazao hayo, ambapo mradi huo, pamoja na mambo mengine, pia utahusisha ujenzi wa kiwanda cha kuzalisha bidhaa kwa mazao ya bahari.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.