Afisa uandikishaji Halmashauri ya Jiji la Tanga Daudi Mayeji amesema zoezi la uboreshaji katika daftari la kudumu la mpiga kura kwa awamu ya mwisho linatarajiwa kuanza tarehe 17/6/2020 na kumalizika tarehe 20/6/2020.
Daudi Mayeji amesema hayo wakati wa zoezi la kuwaapisha wasimamizi watakao simamia uboreshaji wa taarifa katika daftari la kudumu la mpiga kura .
Pia Mayeji amewaasa wasimamizi kuzingatia viapo walivyoapa ikiwa ni jkuwa wasiri katika kazi wanayoenda kuifanya pamoja na kujotoa uanachama .
:Leo mkula kiapo cha kutunza siri pamoja na kiapo cha kujitoa uanachama kwa maana mnatakiwa kuweza kufanya kazi kwa siri pamoja na kutoa haki kwa kila mtu na zoezi hili la uboreshaji taarifa katika daftari la kudumu kla mpiga kula linaanza tarehe 17 mpaka 20 ya mwezi huu wa 6 /2020.Alisema Afisa uandikishaji Halmashauri ya Jiji la Tanga Daudi Mayeji
Mbali na hayo Mayeji alifafanua marekebisho ambayo yatafanyika ni pamoja na kurekebisha taarifa kwa Yule ambaye zimekosewa ,majina kukosewa na tarehe ya kuzaliwa .
Sambamba na hayo pia Mayeji ametoa rai kwa wananchi kujitokeza kurekebisha taarifa zao ilim kuweza kupata nafasi ya kupiga kura kuwachagua viongozi wanaowapenda .
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.