• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Staff Mail |
    • Malalamiko |
Tanga City Council
Tanga City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Tanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Usafi wa Mazingira
      • Mipangomiji na Maliasili
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jiamii na Vijana
      • Maji
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Manunuzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
    • Kata
    • Mitaa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Sekta ya Utalii
    • Sekta ya Madini
    • Sekta ya Elimu
    • Sekta ya Viwanda
    • Maeneo ya Nyumba na Makazi
    • Sekta ya Misitu na Mashamba ya Miti
    • Sekta ya Uvuvi
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Usafi na Mazingira
    • Maji
    • Ardhi na Maliasili
    • Ujenzi na Miundombinu
    • Uwezeshaji Wananchi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Uchumi, Afya na Elimu
      • Kamati ya Mipango Miji na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Siku za Kumuona Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi Iliyoidhinishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Kanuni
    • Fomu Mbalimbali
    • Taratibu
    • Mpango Mkakati
    • Majarida
    • Taarifa za Miradi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
  • TangaTV

UBALOZI WA JAPAN WAJENGA MADARASA 6 YA SHULE YA MSINGI MWAKIDILA

Imewekwa: July 6th, 2018

Shirika la Maendeleo ya Wanawake wa mkoa wa Tanga (Tanga Women Development Initiative - TAWODE) chini ya Mwenyekiti wake Mhe Ummy Mwalimu (Mb.) leo wameweka saini Mkataba wa Ujenzi wa Madarasa 6 ya Shule ya Msingi Mwakidila, iliyopo kata ya Tangasisi, katika jiji la Tanga. Msaada huo wenye thamani ya Dola za Kimarekani 84,000 (takriban shilingi za kitanzania milioni 188) umetolewa na Serikali ya Japan kupitia Ubalozi wa Japan nchini Tanzania kufuatia maombi ya Mwenyekiti wa TAWODE Mhe Ummy Mwalimu ya kuunga mkono Jitihada za Serikali za kuboresha  Miundombinu ya Elimu ya Msingi na Sekondari katika Jiji la Tanga.

Akiongea wakati wa hafla hiyo

Mheshimiwa Masaharu Yoshida, Balozi wa Japan nchini Tanzania amesema, Serikali ya Japan inatoa fedha hizo ili kusaidia Maendeleo ya Elimu kwa Jiji la Tanga ili kutatua tatizo la mrundikano wa wanafunzi madarasani. Mheshimiwa Balozi Yoshida ameitaka TAWODE kuhakikisha Mradi huo unatekelezwa kikamilifu na kukamilika kwa wakati.

Mgeni Rasmi katika Uzinduzi huo Mheshimiwa Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Tanga ameushukuru Ubalozi wa Japan kwa kukubali ombi lao la kufadhili ujenzi wa madarasa ya Shule ya Msingi Mwakidila ambayo ina wanafunzi zaidi ya 1,400 kulinganisha na madarasa machache yaliyopo na hivyo kusababisha mrundikano mkubwa wa wanafunzi. Mhe Ummy alieleza kuwa Ongezeko la wanafunzi limechangiwa na uamuzi mzuri wa  Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe Rais, Dr. John Pombe Magufuli wa kutoa Elimu Bure. Na hivyo wakati Serikali ikiweka jitihada kubwa za kuboresha miundombinu ya Elimu katika Halmashauri mbalimbali kote nchini bado zipo changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa madarasa. Hivyo wao kama sehemu ya wanajamii wa Jiji la Tanga waliona wana wajibu wa kuunga mkono Serikali kwa kutafuta vyanzo vingine vya fedha ili kuwezesha Elimu ya Msingi mpaka kidato cha nne kutolewa Bure bila vikwazo vyovyote.

Mhe Ummy alieleza kuwa Fedha zilizotolewa na Ubalozi wa Japani ni za Jamii ya wanaTanga, kwa Maendeleo ya Tanga. Hivyo Shirika la TAWODE kwa kushirikiana na Serikali kupitia Halmashauri ya Jiji la Tanga itahakikisha msaada huu unatumika kikamilifu na mradi kukamilisha kwa wakati ili kupunguza changamoto ya mrundikano wa wanafunzi madarasani.

Kwa upande wake, Mhe Selebosi Mustafa Mhina, Meya wa Jiji la Tanga ameushukuru Ubalozi wa Japani kwa kufadhili ujenzi wa madarasa hayo. Na pia amemshukuru na kumpongeza Mhe Ummy Mwalimu kwa kuwa nao bega kwa bega katika kusukuma mbele maendeleo ya Wananchi wa Jiji la Tanga hasa katika Sekta ya Afya  na Elimu. Mhe Meya pia amemkaribisha Balozi wa Japan kutembelea Tanga ikiwemo Shule ya Sekondari Japani iliyojengwa kwa ufadhili wa Serikali ya  Japan.

Matangazo

  • TANZANIA CITIES TRANSFORMING INFRASTRUCTURE AND COMPETITIVENESS (TACTIC) PROJECT IDA CREDIT NO. 7151-TZ. March 09, 2025
  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA JIJI TANGA September 27, 2024
  • TAARIFA YA MSIBA September 18, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 26, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • TANGA: MABORESHO DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KUANZA FEB. 13, 2025

    February 04, 2025
  • MENEJIMENTI WAPONGEZWA UTEKELEZAJI MIRADI, UMALIZIAJI WA VIPORO.

    February 04, 2025
  • AFUA ZA LISHE ZAFANYA VIZURI TANGA JIJI

    January 24, 2025
  • KAMATI YA FEDHA NA UONGOZI YAKAGUA MIRADI.

    January 16, 2025
  • Angalia Zote

Video

Baraza la Madiwani la kwanza 2020
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matumizi ya TEHAMA kwa Jiji la Tanga
  • Kata na Mitaa ya Jiji la Tanga
  • Manual ya mfumo wa FFARS
  • Muongozo wa ugawaji wa kitambulisho cha mjasiliamali
  • Jarida la Mifumo Yetu - Novemba 2018-Januari 2019
  • Kupata leseni ya Biashara
  • Tangazo kuhusu watumishi waliomba vibali vya uhamisho
  • Kuanza Ujenzi na Kupata Kibali cha Ujenzi
  • Kuhusu kupata kibali cha kusafiri nje ya nchi

Tovuti Linganifu

  • Ofisi ya Rais, Ikulu
  • Mfumo wa Kuomba Vibali vya Nje ya Nchi
  • Facebook
  • Twitter
  • Instagram
  • Tanzania Government Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Independent Avenue

    Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga

    Simu ya Mezani: 027 2643068

    Simu ya Mkononi:

    Baruapepe: info@tangacc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.