Wananchi katika Jiji la Tanga wametakiwa kujitokeza katika Uandikishaji na Uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ifikapo tarehe 23 mpaka 29 ya mwezi wa kwanza katika vituo vya kujiandikishia .
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Rose Maro wakati akizungumza na Tanga televisheni .
kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Tume ya Uaifa ya uchaguzi Rose Maro amesema ni vyema kwa mtu mwenye vigezo vya kujiandikisha akajitokeza na kufanya hivyo kwani ni haki yake ya msingi .
“Alhamisi hii tunatarajia kuanza Uandikishaji katika Jiji hili la Tanga kwahiyo wale wote ambao wametimiza umri wa kujiandikisha wanatakiwa kujitokeza ili kuweza kujiandikisha na kuboresha taarifa zao kwani maendeleo yanakuja kwa kumchagua kiongozi anayefaa na bila kujiandikisha huwezi kumchagua yule anayekufaa “,.Alisema kaimu mkurugenzi msaidizi wa tume ya taifa ya uchaguzi Rose Maro
Kaimu huyo ameongeza kuwa kwa wale wote waliopoteza kadi zao za kupigia kura na zile zikatika wasisite kujitokeza ili kuweza kupata kadi nyingine .
Kwa upande wake Afisa Uchaguzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi Daniel Kalinga ameziainisha adhabu ambazo mtu atazipata endapo hatafuata Sheria kwa kujiandikisha zaidi ya mara moja .
“Ieleweke katika zoezi hili linaloendeshwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi tunapewa kadi palepale lakini ni kosa kujiandikisha zaidi ya mara moja tunaomba waweze kujiandikisha kwenye kituo kimoja kwani unaweza ukalipa faini ya shilling laki moja hadi laki tatu au kifungo au vyote kwa pamoja “,.Alisema Afisa uchaguzi kutoka tume ya Taifa ya Uchaguzi Daniel Kalinga
Uandikishaji pamoja na Uboreshwaji wa taarifa katika daftari la kudumu la wapiga kura katika Jiji la Tanga unatarajia kuanza tarehe 23 mpaka 29 ya mwezi huu,Wananchi wanatakiwa kujitokeza ili kuweza kupata nafasi ya kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu .
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.