Katibu Tawala wa mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi amewaasa wananchi wa Jiji la Tanga kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la orodha la wapiga kura ili waweze kupata nafasi ya kuchagua viongozi wanaowataka .
Mhandisi Zena ameyasema hayo wakati alipokuwa akijiandikisha katika daftari la orodha la wapiga kula katika mtaa wa Raskazoni amesema sifa ya mpiga kura lazima awe amejiandikisha .
“Msikubali mtu yeyote akawashawishi au akawadanganya kwamba ukiwa na kitambulishi cha kupigia kura basi tayari wewe unahaki ya kupiga kura ni lazima ujiandikishe katika mtaa wako “,.Alisema Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Zena Saidi
Kwa upande wake mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Daudi Mayeji amesema katika vituo hakuna foleni ndefu ambayo itamfanya mtu akakaa kwa muda mrefu hivyo wananchi wajitokeze kwa wingi kwani kujiandikisha ni haki yako ya msingi .
Mkurugenzi huyo ameendelea kuwasisistiza wananchi wa Jiji la Tanga kufuata taratibu za uandikishaji ikiwa ni pamoja na kujiandikisha mara moja katika mitaa yao wanayokaa ili kutopoteza sifa za kupiga kura .
“Ukijiandikisha zaidi ya mara moja ni kosa la kisheria na hatua kali zitachukuliwa kwako ni vizuri kila mwananchi akatumia fursa hiyo kwenda kujiandikisha ili aweze kutumia haki yake kupiga kura “,.Alisema Daudi Mayeji Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga
Mayeji amesema vituo vya kujiandikishia vinafunguliwa saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni hivyo wananchi wananamuda mrefu wa kujitokeza na kujiandikisha hakuchukui muda mrefu .
Uandikishaji katika daftari la orodha ya wapiga kura umeanza rasmi tarehe 8 utamalizika tarehe 17 ya mwezi huu wa 9 hivyo wananchi wote jitokezeni wa wingi kujiandikisha ili kuweza kupata viongozi watakaoleta maendeleo katika mitaa yenu .
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga akijiandikisha katika daftari la orodha ya wapiga kura
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.