Wananchi Jijini Tanga wametakiwa kujiunga katika mapambano ya kifua kikuu ili kuweza kutokomeza ugonjwa huo kwani kuna umuhimu wa kuunganisha nguvu ili kuweza kukabiliana na kifua kikuu .
Akizungumza na tanga television ofisini kwake mratibu wa kifua kikuu na ukoma Mkoa wa Tanga Dkt Raphael Mumba amesema ni vyema kila mmoja akashiriki katika kupamabana na kupiga vita ugonjwa huu kwa kuwaunga mkono watoa elimu katika ngazi ya jamii ili kuendeleza mapambano ya ugonjwa huo.
“Naisihi jamii kujiunga na mapambano haya dhidi ya kifua kikuu vita hii ni ya watu wote na inahusisha makundi yote ya kijamii “,.Alisema mratibu wa kifua kikuu na ukoma Mkoa wa Tanga Dkt Raphael Mumba
Dkt Mumba amesema ni vyema mtu akishaona anadalili za ugonjwa wa kifua kikuu akafika haraka katika kituo cha afya ili kuweza kupewa matibabu kwa haraka lakini jamii kushirikiana na watoa huduma katika ngazi ya jamii pindi wanapotoa elimu ya kupiga vita ugonjwa huo .
Kwaupande wake mchungaji Warehema Chamshama ameeleza namna wao kama viongozi wa dini wanavyoshirikiana na wataalam hao kwa kuelimisha jamii kutowanyanyapaa wagonjwa wa kifua kikuu.
“Sisi kama viongozi wa dini kwa kushirikiana na wataalamu hawa huwa tunapita katika vituo mbalimbali na katika mitaa na kuwaelimisha watu kuacha kuwanyanyapaa wagonjwa wa kifua kikuu “,.Alisema Mchungaji Warehema Chamshama
Tarehe 24 mwezi wa 3 ni siku ya kifua kikuu duniani ambayo huazimishwa kwa kutoa elimu kwa jamii ili kuweza kuelewa ugonjwa huo dalili pamoja na namna ya kujikinga na ugonjwa huo .
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.