Maadhimisho ya situ ya Mazingira Duniani 2019 katika jiji la Tanga yamefanyika shule ya sekondari Kimono kata ya Mzizima ikiwa na kauli mbiu "Tumia Mifuko mbadala wa Plastiki kwa Ustawi wa Afya, Mazingira na Maendeleo ya Uchumi."
Katika maadhimisho hayo Mkuu wa wilaya ya Tanga Mh Thobias Mwilapwa ambaye amesema ni maruku kwa mtu yeyote kutumia mifuko ya plastikI maarufu kama Rambo kutokana na madhara yanayopatikana katika mifuko hiyo, amesema hayo katika maadhimisho ya kilele cha siku ya mazingira duniani yenye kauli mbiu "Tumia mfuko mbadala wa Plastiki kwa Ustawi wa Afya, Mazingira na Maendeleo ya Uchumi" yaliyofanyika shule ya Sekondari Kiomoni iliyopo kata ya Mzizima jijini Tanga.
Mhe.Mwilapwa amesema kuwa utunzaji wa mazingira uplekea kuleta uoto wa asili ambio ni muhimu kwa hewa inayovutwa na kupunguza hali ya joto, pia kulinda vyanzo vya maji ili kuepuka uhaba wa maji na kurudisha nyuma jitihada za maendeleo viwanda.Pia amezitaka shule za sekondari kuwa mfano na kufanya kampeni za kuokota hiyo popote ilipo na kupelekwa mahali palipo chaguliwa na Halmashauri ya jiji la Tanga na kuhifadhiwa kwa ajili ya kupelekwa mahali maalum kwa shughuli ambayo itabuniwa.
Aidha Mratibu wa mradi wa kunusuru vyanzo vya Maji(SLM Project) Mhandisi Maximillian Sekera amesema atawapatia klabu ya Mazingira ya shule ya Kimono Tsh.Mil.5 za mafunzo ya mazingira pamoja na kuwajengea gata ya kuvunia majo ya mvua na kuweka tendí Mkubwa la majo ili kuweza kumwangilia Bustani zao na miti iliyopandwa.
Hata hivyo amesema ifikapo tarehe 1 juni 2019 wilaya ya Tanga itatekeleza agizo lililotolewa na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa kwa kutoa elimu juu ya matumizi ya mfuko mbadala wa plastiki na kuokota mifuko yote iliyopigwa marufuku.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.