Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mustapha Seleboss amewaasa wananchi wa Jiji hilo kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini ili kuendelea kuvitangaza na kujifunza mambo yanayopatikana katika vivutio hivyo .
Mstahiki Meya ameyasema hayo katika uzinduzi wa kipindi cha utalii cha Tanzania yetu kilichozinduliwa katika ukumbi wa Tangamano ambapo amesema ni muhimu kwa watanzania wenyewe kutangaza utalii wa nchi yao na si kusubiri kutangaziwa na watu wengine.
“Huu ni utamaduni wa kujivunia watanzania na hatutakiwi kusubiri wenzetu waje kufanya utalii tunapaswa kufanya utalii kwenye vivutio vyetu lakini kitu kizuri na sisi watu wa tanga tunatakiwa kuonesha utalii wetu katika halmashauri ya Jiji letu kwaiyo niwapongeze tanga tv kwa kuanzisha kipindi hiki kwani naimani watu watajifunza mengi kuhusu utamaduni wa Tanga na na sehemu nyingine “,.Alisema Mstahiki wa Jiji la Tanga Mustapha Seleboss
Nae Mkurugenzi wa Halmashaurii wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji amewaasa waandishi wa vyombo vingine vya habari kuwa na ushirikiano wa kutosha ili kuweza kuitangaza zaidi tanga na kuhabarisha jamii kuhusiana na utalii wa Nchi pamoja na Jiji la Tanga .
“Tanga televisheni ni kituo kinachotoa huduma kwaiyo niwaombe wananchi waendelee kuangalia Tanga televisheni na kufahamu vitu vinavyotokea katika Jiji hili na pia vyombo vingine vya habari vinavyotoa huduma kwa jamii viendelee kuhabarisha watanzania kutembelea hifadhi zetu “,.Alisema Daudi Mayeji Mkurugenzi wa Jiji la Tanga
Kwa upande wake Mkuu wa kituo cha matangazo cha Tanga Televisheni Tusa Daniel ameeleza kazi kubwa ya kituo hicho kuwa ni kutoa elimu,kuhabarisha , pamoja na kuburudisha jamii .
“Uanzishwa wa kipindi cha Tanzania yetu ambacho leo kinazinduliwa kinalengo la kuhamasisha watanzania kujenga utamaduni wao wakufanya utalii katika hifadhi mbalimbali za taifa nchi kwetu Tanzania “,.Alisema Mkuu wa Kituo cha Matangazo cha Tanga televisheni Tusa Daniel
Kipindi cha utalii cha Tanzania yetu kilichoanzishwa na kituo cha matangazo cha Tanga televisheni kina lengo la kuhamasisha utalii kitarushwa kila siku ya Jumanne saa 5 asubuhi na kurudiwa siku ya Jumamosi saa 5 asubuhi .
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.