Afisa elimu Msingi wa Halmashauri ya jiji la Tanga Khalifa Shemahonge amesema wastani wa ufaulu kwa wanafunzi wa darasa la saba kwa mwaka 2019 umepanda kwa 89.1% tofauti na miaka ya nyuma ambapo kwa sasa Jiji la Tanga limeshika nafasi ya 11 kitaifa .
Shemahonge amesema hayo wakati alipotembelewa na tanga television Ofisini kwake ambapo amesema hali ya ufaulu kwa sasa imesababishwa na jitihada walizokuwa wakizifanya ikiwa ni pamoja na wanafunzi kukaa kambi kipindi cha likizo.
“ukilinganisha miaka mitano ya nyuma na sasa kwakweli tumepiga hatua kubwa sana na yote hiyo inasababishwa na jitihada tulizokuwa tumeziweka sisi kuhakikisha tunafanya vizuri lakini pia tumejaribu kupanga ufaulu kikata na kuangalia ni kata zipi ambazo zimeweza kufanya vizuri zaidi ambapo kuna kata tatu ndio zimefanya vizuri zaidi Kata ya Usagara ufaulu wa 181,Magaoni 174 na kata ya central ni 172 na tukiangalia kata hizi zimeongezewa nguvu na shule za binafsi “,.Alisema Afisa elimu Msingi wa Halmashauri ya jiji la Tanga Khalifa Shemahonge
Aidha Shemahonge amewataka Madiwani kushirikiana vyema na walimu ikiwa ni pamoja na kufuatilia maendeleo ya wanafunzi pamoja na ufundishaji wa walimu ili kuweza kuinua sekta ya elimu .
Sambamba na hilo shemahonge amewataka wazazi kushirikiana vyema na walimu pindi wanapoona vitendo vya ukatili kwa wanafunzi kwani vinachangia kwa asilimia kubwa kushuka maendeleo ya taaluma kwa wanafunzi .
Pia shemahonge ametoa wito kwa wazazi kuwapeleka watoto ili wapate elimu kwani kwasasa elimu inatolewa bure bila malipo yeyote .
Afisa elimu Msingi wa Halmashauri ya jiji la Tanga Khalifa Shemahonge akiongea na waandishi wa habari kuhusu matokeo ya darasa la saba
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.