Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela amewataka Wananchi kutunza na kuvilinda vifaa vinavyotolewa na wadau mbalimbali kwaajili ya kujikinga dhidi ya ugonjwa wa corona na kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo.
Akizungumza na Wananchi hao mara baada ya kukabidhiwa vifaa kwaajili ya kunawa mikono kwa maji tiririka vilivyotolewa na kiwanda cha TPPL maarufu kama podoa kilichopo Jijini Tanga Shigela alisema kuna baadhi ya watu wamekuwa hawavitumii kama inavyotakiwa
“Nishukuru sana TTPL kwa msaada huu wa madumu 5 ambayo mmeyatoa kwa Jiji letu la Tanga kwa ajili ya usafi kwani yatasaidia katika kukabiliana na hili janga la Corona katika Mkoa wetu “Alisema Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela
Aidha Shigela aliwataka wananchi wa Mkoa wa Tanga kufuata taratibu zinazotolewa na wataalamu mbalimbali wa afya kama kunawa mikono na kuepuka misongamano ili kuendelea kukabiliana na ugonjwa wa Corona .
Sambamba na hayo Shigela aliwataka wananchi kuweza kutoa taarifa pindi wanapoona mtu mwenye dalili za virusi vya corona ili kuweza kudhibiti maambukuzi yasiendelee kuenea kwa watu wengine .
Kwa upande wake mwakilishi wa kiwanda cha ttpl aliweza kueleza lengo la kutoa msaada huo ni kuweza kuunga mkono juhudi za Serikali katika kukabiliana na ugonjwa wa Corona ambapo madumu hayo yataweza kusaidia sehemu ambazo zina mizunguko ya watu wengi ikiwemo stendi ya Ngamiani ,Hospitali ya Bombo ,stendi ya mwembemawazo ,soko la makorora ,pamoja na soko la Mgandini .
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.