Septemba 21 ni siku ya Amani Duniani, nchini Tanzania maadhimisho hayo yamefanyika kitaifa mkoani Kilimanjaro huku katika Wilaya ya Tanga maadhimisho hayo yakifanyika katika uwanja wa ofisi ya mtendaji kata ya Kiomoni.
Kauli mbiu kwa mwaka huu ikiwa ni "AMANI YETU, MAENDELEO YETU"
Mkuu wa wilaya ya Tanga Mhe. Hashim Mgandilwa ndiye aliyekuwa mgeni rasmi, na akayatumia maadhimisho hayo kuwasisitiza wananchi jukumu la kulinda Amani na usalama katika maeneo Yao Kwa kushirikiana na jeshi la polisi huku wakiendelea kutoa taarifa na kuibua wahalifu waliopo katika maeneo yao
Mgandilwa amewataka wazazi kuwalea watoto wao katika malezi Bora na kuwaepusha kujiunga na makundi ya wahalifu kwani asilimia kubwa ya makundi ya ukatili imeonekana kuwa ni watoto kuanzia umri wa miaka 13, na kuwafichua watu wote wanaosababisha Amani kutoweka
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.