Wakazi wa mitaa itakayonufaika na mradi wa BOOST unaoboresha mazingira ya upatikanaji wa fursa sawa katika ujifunzaji bora wa Elimu ya Awali na Msingi katika Jiji la Tanga kwa mwaka huu wa fedha 2022/2023, wameeleza kufurahishwa kwao na ujio wa mradi huo utakaowawekea mazingira mazuri watoto wawapo shuleni.
Wakazi hao wameeleza hisia zao na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jinsi anavyotoa umuhimu mkubwa katika elimu kwa kuelekeza fedha nyingi kwa ujenzi wa shule mpya, ukarabati wa shule kongwe, mabweni, vyoo na miundombinu mingine huku akitoa ajira kwa walimu.
"Kwa mfano Mama alitoa Billion nyingi kujenga vyumba 8000 vya kuwapoke wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka huu, na fedha za mambo ya sherehe (Sherehe za Uhuru 9 Desemba 2022) akasema zikajenge mabweni kwa wenye mahitaji maalum" alisisitiza mkazi mmoja wa kata ya Duga.
Katika kuhakikisha zoezi la utekelezaji wa mradi wa BOOST linafanyika vizuri, Kamati ya utekelezaji ngazi ya Halmashauri imeendelea na mikutano yake kwa mitaa yenye miradi kwa lengo la kuutambulisha mradi, ambapo katika siku ya Jumatano, Mei 10, 2023, kamati ilifanya mikutano katika shule ya Msingi Msala iliyopo mtaa wa Masiwani Shamba, Kata ya Masiwani na Shule ya Mapambano, iliyopo mtaa wa Swahili, Kata ya Magaoni, ambapo katika shule hizo, kila moja itajengewa vyumba vitatu vya madarasa, na matundu ya vyoo, Msala ikipata matundu 6, na Mapambano matundu 3.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.