Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela amewaasa wananchi wa Jiji la Tanga kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la orodha la wapiga kula ili waweze kuwachagua viongozi wanaowafaa .
Shigela amesema hayo wakati alipokuwa akijiandikisha katika mtaa wa Raskazone amesema ni vyema wananchi wakajiandikisha mapema kusubiri muda wa kupiga kura utakapowadia waweze kupiga kura .
“Uandikishaji katika Jiji la Tanga unaendelea vizuri kwani watu wanajitokeza kujiandikisha mpaka leo 34% ya watu wamejiandikisha sina budi kuwasii wananchi ambao bado hawajajiandikisha kujitokeza kwani ni vyema wakachagua wenyewe na sio kusubiri kuchaguliwa ukichaguliwa unakosa haki ya kumchagua uliyekuwa unamtaka “,.Alisema Martine Shigela Mkuu wa Mkoa wa Tanga
Shigela amesema muda wa vituo kufunguliwa kwaajili ya kujiandikisha kuanzia saa 2:00 asubuhi mpaka saa 12:00 jioni na kujiandikisha hakuchukui muda mrefu ili tarehe 24 mwezi wa 11 washiriki kuchagua viongozi wao wa mitaa .
Kwa upande wake msimamizi wa uchaguzi wilaya ya Tanga Ramadhani Possi amesema hali ya hewa ndio kikwazo kikubwa kinachosababisha watu kutojitokeza kwa wingi katika vituo vyao vya kujiandikishia .
“Tatizo kubwa ambalo linasababisha watu wasijitokeze kwa wingi kwenda katika vituo kujiandikisha ni hali ya hewa kumekuwa na mvua zinazoendelea kunyesha kuanzia tulivyoanza zoezi hili kama hali ya hewa itakuwa vizuri tunatumaini watu wengi watajitokeza kujiandikisha “,.Alisema Ramadhani Possi msimamizi wa uchaguzi Wilaya ya Tanga
Zoezi la uandikishaji katika daftari la orodha ya wapiga kura limeanza rasmi tarehe 8 na linamalizika tarehe 17 ya mwezi huu wa kumi hivyo wananchi mnapaswa kujiandikisha kwani kura yako moja ndio maendeleo ya mtaa wako na Taifa kwa ujumla.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela akipeana mkono na waandikishaji katika kituo cha Raskazoni
Msimamizi wa uchaguzi Wilaya ya Tanga Ramadhani Possi akiwaasa wananchi kujitokeza katika uandikishaji katika daftari la orodha ya wapiga kura
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.