Mkuu wa Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa amewataka Wananchi wanaoishi mipakani kutokuwaingiza watu kinyemela na watoe taarifa katika mamlaka husika na kuchukua tahadhari pindi wanapoona mtu mwenye dalili za ugonjwa wa corona.
Mwilapwa amesema hayo wakati akitoa wito kwa wananchi kuweza kufuata elimu wanayopewa na Wadau wa afya ili kuweza kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Corona huku akiipongeza Halmashauri ya Jiji la Tanga kupitia idara ya afya kwa kutoa elimu kwa wananchi katika mikusanyiko ya watu.
"Huku mpakani kuna tabia ya watu kuingiza watu kinyemela maeneo ya pongwe kunavijana waendesha bodaboda tumeweza kupata taarifa kuwa wanawachukua watu Wakishachukua wanalipwa tumeshakamata watu sita na bodaboda sita watu waache mara moja",.Alisema Mkuu wa Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
Sambamba na hayo pia Mwilapwa ametoa wito kwa wananchi wa Jiji la Tanga kuchukua hatua mapema ikiwa ni pamoja na usafi na kuacha vitu ambavyo vinaweza kusababisha kuambukizana gonjwa hilo kama kukumbatiana.
Pia amewataka wananchi kuacha kuchukuki utani katika ugonjwa huo kwani ni hatari na naweza chukua maisha ya watu kama wasipokuwa makini na elimu zinazotolewa.
Hayo yanakuja baada ya Waziri wa Afya maendeleo ya jamii jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu baada ya kutangaza tarehe 16 mwezi wa 3 kuwa Tanzania amepatikana mgonjwa mmoja mwenye maambukizi ya ugonjwa huo.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.