Katika kuhakikisha uchumi wa Nchi unaimalika wadau mbalimbali wa wakiwemo Madiwani ,Wakuu wa idara mbalimbali ,Mashirika pamoja na wafanyabiashara Jiji Tanga wamekutana ili kupitia mkakati wa uendelezaji wa uchumi katika Jiji hilo.
Akifungua warsha hiyo Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mustapha Seleboss amewataka wadau kuangalia namna gani wanaweza kuikwamua Tanga kiuchumi ili kusonga mbele zaidi.
"Tunahaja ya kuona bahari tunaitumiaje katika suala la kujenga viwanda vya kisasa na mitambo mikubwa kwasababu Tanga tumebarikiwa kuwa na bahari ili kuwasaidia wavuvi wanaondokana na umasikini na kuona tunaisaidia Tanga kusonga mbele ya hapa tulipo"Alisema Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mustapha Seleboss
Sambamba na hayo Mstahiki Meya amewashauri wadau hao kuangalia ni wapi kwenye mapungufu ili kuweza kurekebisha na kuboresha zaidi .
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya uchumi Afya na Elimu Shiloow Abdulrahman amewaasa wadau hao kuwa wabunifu katika kuanzisha biashara zao.
"Tatizo kubwa la watu wanakopy na kupest mtu akitaka kuanzisha biashara anaangalia mwenzake kaanzisha nini na yeye anaiga matokeo yake Tanga inashuka katika maendeleo"Alisema Shiloow Abdulrahman
Nae Mshauri kutoka Shirika la NIRAS Donald Liya amewaasa wafanyabiashara hao kuwa na nia ya dhati katika kutekeleza jambo hilo ili kusaidia kuinua uchumi wa Tanga .
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.