Mstahiki Meya wa Jiji la Mustafa Seleboss amesema Mkoa wa Tanga umetoa shilingi milioni mbili na kumkabidhi bondia Hassan Mwakinyo anayetarajia kufanya pambano la masumbwi novemba 29 jijini Daresalaam kama sehemu ya kumuunga mkono.
Pambano hilo la masumbwi kati ya bondia wa Tanzania Hassan Mwakinyo na mfilipino Arnel Tinampay linatarajiwa kufanyika kwenye uwanja wa uhuru jijini Daresalaam.
“Tulisema pamoja na kumuaga na kumpasapoti Mwakinyo kwa wale wanaotaka kwenda kwa ajili ya ushangiliaji na mimi nitatoa milioni moja lakini michango mingine bado inaendelea “,.Alisema Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela
Nao baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Tanga wameendelea kuwasisitiza Wananchi wa Tanga kuendelea kuwa na matumaini na bondia huyo .
“Tunatarajia Mwakinyo atarudi na ushindi na yeye kwa upande wake aone kuwa tumempa heshima kubwa sana na kazi yetu kubwa ni kuonesha kwamba tupo pamoja “,.Walisema viongozi hao
Pia Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mustafa Seleboss amewataka wakazi wa Tanga kuendelea kutoa ushirikiano kwa bondia Hassan Mwakinyo ili kuweza kumpa nguvu ya kupambana na hatimaye kurudi na ushindi nyumbani.
Kwa upande wake bondia Hassan Mwakinyo ameushukuru uongozi wa Mkoa wa Tanga kwa kumuchangia na kuahidi kufanya vizuri katika pambano lake linalotarajia kufanyika siku ya ijumaa ya tarehe 29/11/2019 katika viwanja vya uhuru Jijini Dar es salaam .
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.