Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela ameishukuru Benki Kuu ya Tanzania kwa kuja Tanga na kutoa elimu ya shughuli zinazofanywa na Benki hiyo sambamba na kutambua fursa mbalimbali zilizopo katika Mkoa wa Tanga kwa ujumla.
Shigela amesema kuwa kupitia elimu hiyo iliyotolewa na Benki Kuu itasaidia kuweka mikakati katika Sekta ya Umma pamoja na Sekta Binafsi ili kujua ni namna gani ya kuboresha maisha ya watu na kuweza kuinua Uchumi wa mtu mmoja na Taifa .
“Ni jambo zuri kwasababu sisi sikuzote tunaangalia ngazi ya Taifa na Nchi yetu inafanya vizuri kwenye mapato pia inafanya vizuri kwenye makusanyo kwaiyo ukiyaboresha maisha ya watu unakuwa umeboresha Nchi na mtu mmojammoja “,.Alisema Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela
Shigela amesema chini ya Uongozi wa Rais Dkt John Magufuli umeifanya Tanga kurudi kwenye nafasi yake kwa uchangiaji mzuri wa pato la Taifa .
“Viwanda vingi vikubwa historia yake ni Tanga ,historia ya shule ipo Tanga ,Reli nayo ni Tanga ,Bandari i Tanga sasa kwanini tusirudi kwenye nafasi yetu “,. Alisema Martine Shigela
Kwa upande wake Meneja wa Idara ya Uchumi Benki kuu kanda ya kaskazini Dr Wilfred Mbowe amesema ni sehemu ya sera ya Benki Kuu kukutana na wadau lakini pia na washirika wake na kuelezea mambo mbalimbali yanayohusu Uchumi jinsi unavyoendelea.
“Hapa tulikuwa tunahudhuria kikao cha ushauri cha Mkoa wa Tanga lakini pia kufafanua fursa ambazo zinapatikana katika mkoa huu na zinahusiana na masoko”,.Alisema Dr Wilfred Mbowe
Lengo kuu la serikali ni kuwafanya wadau wafahamu hayo masoko na pia wanaweza wakashauri nini kifanyike .
Washiriki mbalimbali waliojitokeza kupata elimu inayotolewa na benki kuu
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.