Mkuu wa Wilaya ya tanga Thobias Mwilapwa ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuwa na ushirikiano katika kutoa taarifa pindi wanapoona watu wakiingia kinyemela katika Wilaya ya tanga na kuwataka kuendelea kuzingatia masuala ya usalama kwa kuchukua tahadhari zinazotakiwa .
Akizungumza na tanga televisheni Mkuu wa wilaya hiyo Thobias Mwilapwa aliwatoa wawasi wananchi katika kipindi hiki cha sikukuu za pasaka kuwa watahakikisha wanaimarisha ulinzi kwenye nyumba za ibada ,Fukwe na kuwaasa wananchi kutokaa katika sehemu zenye mikusanyiko .
“Nianze kwa kuwatakia heri ya sikukuu ya pasaka wakristo wote na nipende kumshukuru mungu kuwa mpaka sasa Tanga hatuna mgonjwa yeyote mwenye maambukizi ya virusi vya Corona na yote hiyo ni kwasababu wananchi wanaonesha mshikamano wa kutosha kwa kuwafichua wageni wanaoingia kwa njia za kinyemela niwashukuru sana na niwatoe wasisi kuwa katika masuala ya usalama kwa kipindi hiki cha sikukuu tumeandaa nguvu kutoka kwa askari itakayozunguka kuhakikisha usalama katika makanisa na sehemu za fukwe “Alisema Mkuu wa Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
Sambamba na hayo Mwilapwa aliwataka wananchi kutambua kila anayewekwa sehemu kwaajili ya uangalizi sio mgonjwa hivyo waache tabia ya kutoroka wakiwekwa huko kwani kwakufanya hivyo wanaweza kueneza ugonjwa kwa watu wengine .
Kwa Upande wake mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji alisema katika kpindi hiki ambacho dunia inaendelea kupambana na ugonjwa wa corona,Halmashauri ya Jiji la Tanga inaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuzingatia maelekezo ya wataalam wa afya.
Mbali na hayo Mkurugenzi huyo aliweza kuwakumbusha wananchi kuwa na amani katika kusherekea sikukuu ya pasaka .
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.