Zoezi la uandikishaji katika dafrati la kudumu la mpiga kura katika Mkoa wa Tanga limeanza hii leo huku tahadhari zote zinazotolewa na wataalamu wa afya kuhusu ugonjwa wa corona zikiwa zimezingatiwa .
Akizungumza na tanga televisheni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Nchini Mh. Jaji Semistocles Kaijage aliweza kumpongeza Afisa mwandikishaji wa Tanga Jiji Daudi Mayeji jinsi alivyochukua tahadhari za ugonjwa wa Corona katika zoezi hilo la uandikishaji.
"zoezi la kuandikishaji katika daftari la kudumu la wapiga kura limeanza vizuri katika mikoa yote kumi na mbili katika mzunguko huu wa kwanza na katika Mkoa wa Tanga naona Tahadhari zote zilizoelekezwa na wataalamu wa afya zinazingatiwa elimu ya mpiga kura katika Jiji hili imetolewa vizuri sana "Alisema Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Nchini Mh. Jaji Semistocles Kaijage
Mbali na hayo pia Mwenyekiti huyo alisema wananchi wa Jiji la Tanga wameonesha mwamko mzuri katika kujitokeza kujiandikisha katika vituo vyao na wameweza kuchukua tahadhari zote .
"Mkurugenzi na watu wako nikushukuru sana kwani mmefanya kazi nzuri sana kwa kuweza kufanikisha jambo hili lakini kwa tahadhari ambazo mmeweza kuzichukua "Aliongeza Mwenyekiti huyo
Pia aliweza kutoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Tanga kuendelea kuzingatia tahadhari zote zinazotolewa na wataalamu wa afya juu ya ugonjwa wa Corona .
(Wananchi nawaomba wawe na uhakika na vituo ambavyo tumeviandaa kwani tahadhari zote zimewekwa na wenyewe niwaombe waendelee kuzingatia tahadhari )Alisema Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
zoezi la uboreshaji daftari la kudumu la mpiga kura awamu ya pili limeanza leo katika mikoa 12 nchini huku ikiwa Mkoa wa Tanga ni Moja kati ya Mikoa hiyo .
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.