Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la tanga Daudi mayeji ameishukuru kampuni ya ASA Microfinance (TANZANIA) LTD kwa msaada wa chakula ambao wametoa kwani utasaidia mashuleni kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula cha mchana kwakuwa muda wa masomo umeongezwa mpaka saa 10:30.
Mayeji alitoa pongezi hizo wakati akipokea msaada huo kutoka kwa kampuni ya ASA Microfinance (TANZANIA) LTD ambapo ameahidi msaada huo utafika kwa walengwa .
“Nawashukuru sana Micrifinance kwa msaada huu kwani hiki chakula tutapeleka katika taasisi zetu za shule kwakuwa muda umeongezwa kwaiyo ambayo imetoa mchele, unga ,sukari,maharage ,mafuta ya kula pamoja na sabuni .wanafunzi wataweza kupata chakula cha mchana na tunaahidi tutafikishwa kwa wanafunzi ili waweze kusoma vizuri “Alisema Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji
Kwaupande wake meneja wa ASA Micrifinance Tanzania limited Afzal Hossain alisema lengo la kutoa msaada huo ni kuhakikisha sekta ya elimu inaenda vizuri.
Nae afisa lishe wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Sakina Mustapha aliishukuru kampuni hiyo kwaajili ya msaada walioutoa kwani umetolewa katika wakati mwafaka ambao wanafunzi ndio wamefungua shule .
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.