Na: Mussa Labani, Dar es Salaam.
Halmashauri ya Jiji la Tanga, kupitia Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, imeshika nafasi ya tisa (9) kati ya Halmashauri 184 nchini, katika utoaji wa taarifa za kazi za Serikali, ikiwemo utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri husika, kufuatia tathmini iliyofanywa na Wizara ya Habari, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa kuangalia namna Wizara, Taasisi, Ofisi za Mikoa na Halmashauri zinavyotoa taarifa kwa umma kwa kipindi cha mwaka 2023/2024.
Akitangaza matokeo hayo, mbele ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, wakati wa Kongamano la Maendeleo ya Sekta ya Habari na Kikao kazi cha Maafisa Habari wa Serikali kinachofanyika Jijini Dar es Salaam, Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO, Bw. Thobias Makoba, amesema tathmini hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa maazimio ya kuimarisha mawasiliano ya Serikali kwa umma, lengo likiwa ni kuwafanya Maafisa Habari kutoa taarifa kwa kina kwa wananchi kuhusu miradi yote ya maendeleo.
Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amewapongeza wote waliofanya vizuri na kupata tuzo, na kuzitaka Halmashauri zilizotunzwa mwaka huu kuendelea kufanya vizuri, na zile ambazo bado, nazo zifanye hivyo.
Aidha Mheshimiwa Rais ameshauri kuboreshwa kwa tathmini hiyo kwa kuweka makundi (category) za upimaji kwa kutenga Halmashauri za majiji, miji, badala ya zote kuwekwa katika kapu moja, huku akiagiza kujumuishwa kwa ushiriki wa sekta zingine, kama ilivyofanya sekta ya maji kupitia Mamlaka ya maji.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.