Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Tanga limekutana leo Alhamisi Jijini hapa kujadili hesabu za mwisho wa mwaka wa fedha 2018/2019.
Akifungua baraza hilo Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mustapha Selebos amesema Halmashauri ya Jiji la Tanga imefikia lengo la mapato yake ya ndani kwa 84% na kuwataka Viongozi pamoja na wakuu wa idara kuongeza juhudi ili kufikia 100% ambayo ndio lengo kuu .
“Kwanza niwashukuru waheshimiwa Madiwani sifa hizi ni zetu sote tumevumiliana sana katika kazi na siri kubwa ya mafanikio haya ni kwenu waheshimiwa Madiwani kwasababu tumeangalia Tanga kwanza”,.Alisema Mustapha Selebos
Mustahiki Meya amesema kuwa viongozi wa Jiji la Tanga wamekuwa na umoja ambao haujaangalia vyama wanavyotoka kitu ambacho ni kizuri katika kuleta maendeleo katika Jiji na Mkoa kwa ujumla .
“Tumeanza vizuri sana lakini tunatakiwa tunapokutana tena tuzungumzie asilimia kubwa zaidi ya hapa tulipo kwahiyo tunaporudi katika maeneo yetu sisi tuwe sehemu ya kuwahamasisha watu kulipa kodi ”,.Alisema Mstahiki Meya
Aidha Mstahiki Meya ametoa wito kwa Madiwani kukagua vitambulisho vya wafanyabiashara wadogowadogo ili kuweza kuwatambua wafanyabiashara wanaofaa kupewa vitambulisho kwani kumekuwa na wafanyabiashara wasiokidhi vigezo vya kumiliki vitambulisho hivyo hususani wavuvi .
Mkutano huo maalumu wa madiwani wakujadili hesabu za mwisho wa mwaka wa fedha 2018/2019, Pia Halmashauri ya Jiji la Tanga imejipanga kuongeza zaidi mapato kwa kuibua vianzia mbalimbali vya mapato ikiwemo mradi wa kufyatua matofali kwa kutumia mashine za kisasa na kuuza matofali hayo kwa wadau mbalimbali kwa mwaka wa fedha 2019/2020
. Madiwani Jijini Tanga wakiwa katika kikao cha mwisho kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
Wakuu wa idara wakiwa makini kusikiliza katika kikao cha mwisho kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.