Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omary ameipongeza Halmashauri ya Jiji la Tanga kwani asilimia 50 ya mapato ya ndani ya Mkoa yanatoka katika Halmashauri hiyo.
Judica aliyasema hayo wakati wa Baraza la Diwani ambapo alisema Mkoa wa Tanga unaitegemea sana Halmashauri ya Jiji la Tanga katika ukusanyaji wa mapato .
“Ukiangali karibu asilimia 50 ya mapato yote ya Mkoa na ukiyajumuisha mapoja na Halmashauri nyingine yanatoka kwenye Jiji la Tanga kwaiyo Jiji la Tanga kwetu tunalipa kipaumbele na tunalitazama sana kwaiyo tukazane kukusaya vyema mapato”Alisema Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omary
Sambamba na hayo pia Judica aliwaomba Madiwani hao kuendelea kusimamia vizuri vyanzo vya ndani vya mapato kwa karibu ili lengo lipate kutimia.
Pia aliwataka viongozi hao kuangalia mapato ambayo bado yapo mikononi mwa wakusanyaji ili yaweze kuingizwa kwenye mfuko kwa kuwa yanahitajika kuingizwa kwenye akaunti maalum .
Mbali na hao aliwasisitiza Madiwani hao kuendelea kuwatumikia wananchi wao bila kuangalia itikadi za vyama ili kuweza kukuza uchumi wa nchi .
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.