Na: Pamela Chauya
Julai 11, 2024.
Wavuvi katika Jiji la Tanga wameendelea kusalimisha zana za uvuvi haramu katika ofisi za kata ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dkt. Batilda Burian, alilolitoa hivi karibuni, ambapo katika Jiji la Tanga, zimebainika Kata tano kuwa na wavuvi wanaotumia zana zilizopigwa marufuku (zana haramu).
Akizungumza na jamii ya wakazi wa mwambao wa pwani ya bahari ya Hindi, ambayo ndiyo inayojihusisha kwa kiasi kikubwa na mazao ya bahari, Afisa Uvuvi kutoka Jiji la Tanga Bw. Aneny Nyirenda, amesema wavuvi sabini na tano ( 75) wamesalimisha zana zao na kuachana na uvuvi haramu kwa ustawi wa rasilimali ya uvuvi katika bahari.
Nyerenda amesema ifikapo tarehe 13 Julai, zoezi litasitishwa katika Jiji la Tanga ili kupisha zoezi la kimkoa huku uchukuaji hatua za kisheria kwa walio kaidi kufuata.
Kwa upande wake mzee Jumbe Akida ameiomba Halmashauri kuwaongezea vijana boti za uvuvi, ili waweze kuachana na uvuvi haramu.
"Vijana Acheni uvuvi haramu, sisi wazee wenu tumevua enzi hizo wala hatukutofautiana na serikali, kuweni waadilifu kwani uvuvi ni kazi inayowapatia kipato" alisema mzee Akida.
Mwarongo ni moja ya kata ambayo wavuvi wameitikia agizo la Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Mkoa kwa kukabidhi vifaa walivyokuwa wakitumia katika uvuvi haramu.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.