Halmashauri ya Jiji la tanga tayari imeshachukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa wa Corona katika maeneo yenye mkusanyiko wa watu ikiwemo katika Ofisi ya Halmashauri, shule za msingi na sekondari pamoja na zanati na vituo vyote vya afya .
Akizungumza na Tanga Televison Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Ramadhani Possi amesema kuwa tayari maelekezo yameshatoka hivyo ni vyema kuchukua tahadhari ya ugonjwa huo.
“Katika Halmashauri yetu tumeshachukua tahadhari katika maeneo mbalimbali ya Jiji letu moja kati ya hatua tulizochukua ni kuhakikisha maeneo yote yale yenye mikusanyiko ya watu tumeweka vitu ambavyo vinaweza vikazuia yale maambukizi “,.Alisema Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Ramadhani Possi
Mbali na maofisi pia Kaimu Mkurugenzi huyo amesema ili kuweza kuwaweka watoto katika hali ya usalama na kuepuka maambukizi katika mashule wameshaweka vifaa hivyo katika mashule hayo .
Kwa upande wake Afisa elimu sekondari Lusajo Gwakisa amewasisitiza walimu kuwa makini kwa maelekezo wanayopewa pamoja na kuwaasa wanafunzi kuwasikiliza walimu wao .
Nae Mganga mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Charles Mkombe amezitaja njia ambazo zinaweza kusaidia kuzuia maambukizi hao kwa kunawa mikono kila wakati ,na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari kabla ya hatari.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.