Mkuu wa Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa amewataka wafanyabiashara kufuata bei elekezi ya sukari iliyopangwa na Serikali na kutoa onyo kwa yeyote atakayekiuka agizo hilo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Mwilapwa alitoa kauli hiyo kutokana na baadhi ya wafanyabiashara wa Jiji la Tanga kuendelea kuuza sukari kinyume na bei ambayo imepangwa na Serikali.
“Siku za hivi karibuni bei ya sukari ilkuwa imepanda sana lakini bado kuna wafanyabiashara ambao bado wamekuwa hawasikilizi maagizo ya Serikali “Alisama hayo Mkuu wa Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
Mwilapwa aliongeza kwa kutoa taarifa ya kuwanasa wafanyabiashara 6 waliokuwa wakiuza sukari kwa bei ambayo haijaelekezwa na wizara ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa .
Sambamba na hayo pia Mwilapwa aliweza kueleza hatua ambazo wao kama kamati ya usalama Wilaya ya Tanga wameweza kuchukua ikiwa ni pamoja na kufuatilia muenendo wa uuzaji wa sukari kwa bei elekezi kama inafuatwa .
Wizara ya viwanda na biashara iliweza kuelekeza bei ya sukari kwa kila Mkoa ambapo katika Mkoa wa Tanga kilomoja ya sukari ni shilingi 2700.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.