Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yameadhishwa leo Juni 16 katika Jiji la Tanga kwa jamii kukumbushwa wajibu wao wa kumlinda Mtoto dhidi ya vitendo vya Ukatili kwa kushiriki kupambana na vitendo hivyo ikiwa ni Pamoja na kufichua kwa kutoa taarifa kwa vyombo husika ili vichukue hatua stahiki.
Akiongea katika maadhimisho hayo, Mkurugenzi wa Jiji la Tanga, Ndg. Sipora Liana, ambaye alikuwa Mgeni Rasmi, amesema jamii ina wajibu wa kushiriki katika ulinzi wa mtoto dhidi ya vitendo vyote vya ukatili dhidi yao.
Ndg Liana pia ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha wakazi wa Jiji la Tanga umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi ifikapo Agosti 23, 2022.
Amesema Sensa ina lengo la kuiwezesha Serikali kupata takwimu za msingi za watu na hali ya makazi ambazo zitasaidia kutunga sera, kupanga na kufuatilia mipango ya maendeleo ya kimkakati inayolenga kukuza ustawi wa nchi na watu wake.
Siku ya Mtoto wa Afrika ilianzishwa na Umoja wa Mataifa UN, na kuanza kuadhimishwa mwaka 1991, na kwa Mwaka 2022 Tanzania imeadhimisha siku hii ikibeba kauli mbiu isemayo TUIMARISHE ULINZI WA MTOTO, TOKOMEZA UKATILI DHIDI YAKE, JIANDAE KUHESABIWA.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.