Na; Mussa Labani, Dodoma.
Timu za Jiji la Tanga zinazoshiriki mashindano ya Shirikisho la Michezo la Serikali za Mitaa yanayoendelea Jijini Dodoma, zimefanikiwa kuongoza makundi yao, na hivyo kusonga mbele kwa hatua ya pili, ambapo timu ya mpira wa miguu wameingia hatu ya 16 bora, huku netball wakiingia robo fainali.
Mwenyekiti wa Timu hiyo Mhe. Selebosi Mustafa amepongeza Uongozi wa Halmashauri kwa uamuzi sahihi wa kuleta timu katika mashindano hayo, na amewaomba wana Tanga kuendelea kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu ili warudi na vikombe.
"Tumekuja kushindana, hatukuja kuwakilisha" Amehitimisha Mwenyekiti huyo.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.