Na; Mussa Labani, Dodoma.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Bw. Said Majaliwa, amezipongeza Timu za Jiji la Tanga zinazoshiriki mashindano ya Shirikisho la Michezo la Serikali za Mitaa (SHIMISEMITA) yanayoendelea Jijini Dodoma, kwa kufanikiwa kuingia hatua ya pili ya mashindano hayo, ambapo timu ya wavulana imefanikiwa kuongoza kundi na kuingia 16 bora, huku wasichana nao wakiongoza kundi lao na kuingia robo fainali.
Mkurugenzi Majaliwa ametoa pongezi hizo alipozitembelea timu hizo, na kuangalia mchezo wa mpira wa miguu kati ya Jiji la Tanga na Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero, uliochezwa katika uwanja wa Shule ya Sekondari Dodoma, na kuisha kwa sare ya 1 - 1.
Majaliwa pia ameishukuru Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa kuandaa michezo hiyo, amesema michezo ya SHIMISEMITA inawakutanisha watumishi wa Serikali za Mitaa na kuwapa nafasi za kuonyesha vipaji vyao, na kwamba wapo wachezaji wazuri kwenye Halmashauri wanaoweza hata kucheza katika timu zenye hadhi ya kimataifa.
Amesema iwapo mwakani mashindano yakiwepo, Jiji la Tanga litashiriki katika michezo mbalimbali na kuhakikisha linabeba vikombe vyote.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.