Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela ametembelea vituo mbalimbali vya uandikishaji katika kata ya magaoni na kuzungumza na wananchi juu ya umuhimu wa kujiandikisha katika daftari hilo.
Shigela amesema zoezi hilo la uandishaji pamoja na uhakiki wa taarifa ni muhimu kwa kila mwananchi kwa kuwa watawapa haki ya wakuchagua viongozi katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika October mwaka huu .
Sambamba na hayo pia shigela ameipongeza serikali ya awamu ya tano kwa kazi nzuri ya kuhakikisha inaimarisha demokrasia ya Taifa kwani ni moja ya ukomavu wa maendeleo katika Taifa .
"Mimi nimetumia nafasi yangu kuja kujiandikisha katika kituo changu cha raskazon mwaka uliopita nilikuwa Dar es salaam na ndio yalikuwa makao yangu sasa baada ya Mhe Rais kunichagua kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga ndio nmekuja kurekebisha taarifa zangu",.Alisema Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela
Pia Mhe Shigela ameendelea kuwakumbusha wananchi ambao bado hawajarekebisha taarifa zao pamoja na kujiandikisha kwenda kufanya hivyo.
Uandikishaji katika daftari la kudumu la mpiga kura katika Mkoa wa Tanga unamalizika hii leo ya tarehe 29 ya mwezi wa kwanza .
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.