Waziri wa Afya maendeleo ya jamii jinsia Wazee na watoto Ummy Mwalimu amesema Serikali imejipanga kukabiriana na ugonjwa wa Corona unaoendelea katika maeneo mbalimbali Duniani ambapo mpaka sasa ugonjwa huo umeripotiwa Kuwepo kenya.
Ummy amesema hayo wakati alipokuwa akizungumza na wananchi Mkoani Tanga katika uzinduzi wa Mradi wa Scalling up Family Planning ambapo amewataka Wananchi wa Tanga kuchukua tahadhari mapema.
"Hatupo tena kwenye kujiandaa Sisi kama serikali kupitia wizara ya Afya sasa hivi tupo katika hatua ya kukabiliana hatuna maandalizi tena tumeshamaliza maandalizi sasa hivi tunakabiriana ",.Alisema Ummy Mwalimu
Sambamba na hayo pia amekitaja kituo Pongwe ambacho kitakuwa ni mahususi kwaajili ya kutibu wagonjwa wa corona katika Mkoa wa Tanga endapo watapatikana.
Kwa upande wake Mganga mkuu wa Mkoa wa Tanga Jonathan Budenu amewataka wananchi wa Mkoa wa Tanga kuepuka kupeana mikono ,kukumbatiana Pamoja na kushika uso mara kwa mara na kutoa taarifa pindi wanapoona mtu mwenye dalili za ugonjwa huo.
"Ushauri wangu kwa watu wa Tanga ni waepuke kupeana mikono kwa kusalimiana , kukumbatiana na kupunguza misongamano"Alisema Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Jonathan Budenu
Nao wananchi wa Jiji la Tanga wameiomba Serikali kuchukua mikakati mapema katika mipaka ya Tanzania na Kenya ili kuweza kuwabaini wagonjwa hao na kudhibiti kuwaambukiza wengine.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.