Mkuu wa mkoa wa Tanga mhe.Martin Shigela ametembelea mradi wa ujenzi wa Hospital na Vituo vya Afya unaondelea katika jiji la Tanga leo ikiwa ni moja kati ya Halmashauri 11 za Mkoa wa Tanga.
Katika ziara hiyo aliyoanza kutembelea kituo cha Afya Mwakidila kinachotarijiwa kuanza kujengwa ambapo kipo hatua za awali za kuanza kujenga msingi , Mkuu wa mkoa amesema kazi ya kuanza kujenga msingi wa kituo hiki cha Afya Mwakidila ianze mara moja ili kuendelea kusogeza huduma ya Afya karibu na wananchi
Mkuu wa mkoa wa Tanga mhe.Martin Shigela pia ametembele ujenzi wa Hospital ya wilaya ya Tanga Masiwani Shamba kufuatilia maendeleo ya ujenzi wa mradi huo unaoendelea “Nimeridhishwa na kasi ya ujenzi wa Hospital ya Wilaya ya Tanga namna unavyoendelea na hatua za ujenzi zilivyofikiwa, naendelea kusisitiza kasi iongezeke ili majengo hayo yakamilike kwa wakati na kutoa huduma iliyokusudiwa” amesema Martin Shigela Mkuu wa Mkoa.
Ujenzi wa Hospitali ya wilaya Tanga umefikia hatua mbalimbali za ukamilishaji ambapo majengo yote yamefikia hatua ya upandishaji lenta, kufikia julai 30 ni matarajio majengo hayo yatakuwa yamekamilika.
Mkurugenzi wa jiji la Tanga Daudi Mayeji amemuahidi Mkuu wa mkoa kuwa ujenzi wa Hospitali ya wilaya na Vituo vya Afya utakamilika kwa wakati na kwa ubora uliozingatiwa,”mhe.Mkuu wa mkoa tunakuahaidi kukamilisha ujenzi wa Hospital ya wilaya na kituo cha Afya Duga kwa wakati na kuanza mara moja ujenzi wa kituo cha Afya Mwakidila kufikia wiki ijayo kitakuwa katika hatua nzuri kwa kasi kubwa tuliyonayo” alisema Mkurugenzi Daudi Mayeji.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.