Julai 2, 2025.
Ikiwa zimebaki siku chache kuelekea maonesho ya wakulima maarufu kama nane nane kwa mwaka huu, yanayotarajiwa kufunguliwa Augosti 1, 2025, Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, Ndg. Rashid Mchatta, amekagua vipando vya mazao na maandalizi ya mabanda ya maonesho kwa Halmashauri za mkoa wa Tanga, vilivyopo ndani ya uwanja wa Mwl. J. K. Nyerere katika Manispaa ya Morogoro.
Katika eneo la Jiji la Tanga, RAS Mchatta alipokelewa na Maafisa wa Halmashauri ya Jiji la Tanga, wakiongozwa na Kaimu Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Jumanne Diwani, na kupokea maelezo namna Jiji la Tanga lilivyojiandaa na maonesho ya mwaka huu.
Mchatta alipongeza maandalizi na kuelekeza juhudi zaidi ziongezwe katika kukamilisha maandalizi, huku alisifu jengo la maonesho la Jiji la Tanga.
Kesho alhamisi Julai 3, 2025, katika uwanja huo, kitafanyika kikao cha Kamati Kuu ya maandalizi ambacho kinahusisha viongozi wakuu wa mikoa, Wilaya na Halmashauri kutoka mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani na Morogoro inayounda kanda ya Mashariki ya maonesho hayo.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.