Halmashauri ya jiji la Tanga imepokea jumla ya sh.Mil.700 kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ikiwa imelenga kuboresha Kituo cha Afya Duga ili kiweze kutoa huduma za afya kwa wananchi wa jiji la Tanga.Hii ikiwa ni mwendelezo wa mpango wa serikali wa maboresho ya vituo vya kutolea huduma za afya.
Katika fedha hizi Mil.500 zimeelekeza kujenga Wodi ya Wazazi, Maabara (Laboratory), Jengo la Upasuaji (Theatre), huku Mil.200 zikitengwa kununua vifaa tiba vya kituo hicho, mradi huu umeanza rasmi kutekelezwa tarehe 02/01/2019 na unatarijiwa kukamilika Mei,2019.ujenzi wa kuboresha kituo hiki cha afya umefikia hatua mbalimbali za ukamilishaji, ambapo jengo la upasuaji, Wodi ya wazazi yamefikia hatua ya lenta na maabara imefikia hatua ya kunyanyua msingi.
Kituo cha afya Duga kinahudumia wagonjwa takribani 800 kwa mwezi, ikiwa ni idadi kubwa hivyo kupelekea Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kutenga na kupeleka fedha kata ya Duga ili kuboresha huduma za afya na kusogeza huduma hiyo karibu zaidi na wananchi.
Jengo la Upasuaji likiwa hatua ya kupandisha lenta.
Jengo la wodi ya wakina Mama likiwa hatua ya Lenta.
Fundi akita amoeba zege kuendelea na ujenzi.
Jengo la maabara likiwa hatua ya kunyanyua msingi.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.