Na: Mussa Labani, Arusha.
Naibu Meya wa Jiji la Tanga, Mhe. Rehema Mhina ameshuhudia utiaji saini wa hati za makubaliano ya ushirikiano kati ya Jiji la Tanga na Shirika lisilo la Kiserikali la Tanzania Horticultural Association (TAHA), linalo jishughulisha na kuendeleza sekta ya horticulture nchini, kwa utoaji wa elimu juu ya uzalishaji na uchakataji wa mazao ya viungo na mengine ya mbogamboga kibiashara.
Mkataba huo umeingiwa siku ya Jumanne, Julai 02, 2024, kwa pande mbili hizo kusaini hati za makubaliano hayo, ambapo kwa upande wa Jiji la Tanga zimesainiwa na Mkurugenzi wa Jiji Dkt. Frederick Sagamiko, na kwa upande wa TAHA akisaini Mtendaji Mkuu Dkt. Jacqueline Mkindi, tukio lililofanyika katika ofisi za Makao Makuu ya TAHA, Jijini Arusha.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.