Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Tanga imetoa masaada wa Chakula katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu YDCP Jijini Tanga lengo likiwa nikuwasaidia watoto hao kupata lishe iliyo bora.
Akikabidhi msaada huo Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa aliwataka wale wote wanaoguswa na jambo hilo kuweza kuwasaidia watoto hao.
“Tuliazimia kwenye kikao chetu cha kamati ya usalama ya Wilaya tutafute namna ya kupata vitu kidogo kutoka kwenye mfuko wetu na tumepata vitu kidogo ili tuje tusaidie kituo hiki tunajua mnafanya kazi kubwa ya kuwalea hawa watoto ili wasijisikia kama wametengwa tumeamua kufanya hivi kama Serikali kuunga mkono juhudi zenu lakini pia Kuwahamasisha wengine kuona umuhimu wa kuwasaidia watoto wetu “Alisema Thobias Mwilapwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga
Mbali na hayo pia amewataka watoto hao kujiona kama watu wengine na kuacha dhana ya kujidharau na kujiona hawafai katika jamii kwani wapo katika nchi ambayo ina amani na demokrasia yenye upendo .
Nae Prisca Joshua ambae ni Afisa utetezi wa kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu cha YDCP Jijini Tanga alishukuru kwa msaada huo .
Pamoja na hayo Bi Prisca aliweza kueleza jinsi wanavyowapa elimu ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa corona watoto hao kwa kuwapatia vipeperushi ili kuweza kujisomea wakiwa majumbani kwao kwani kwa sasa wameruhusiwa kuwa na wazazi wao kutokana na mlipuko wa ugonjwa huo .
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.