Mkuu wa Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ametoa agizo kwa wote waliofungua madarasa ya pembeni na kufundisha Wanafunzi au Wanachuo manyumbani maarufu kama (tution) wafunge mara moja kwani ni kupingana na tamko la Serikali kutokana na kupiga marufuku mikusanyiko ili kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.
Mwilapwa amesema hayo wakati akizungumza na tanga television juu ya watu ambao wamefungua tution ambazo ni mikusanyiko kwani Serikali imewaondoa Wanafunzi Mashuleni ili kuwakinga na maambukizi ya ugonjwa wa corona.
“Zipo habari baada ya vijana kuwatawanya lakini kuna watu wanaendelea kuwakusanya kwenye maeneo fulani kama maeneo ya Burudani ,Vijiwe au Madarasa ya kufundishana yote hiyo sahihi kwasababu tutakuwa tunakwenda kinyume cha mpango wa Serikali ya kuondoa msongamano kama mkakati wa kupambana na ugonjwa wa Corona “,.Alisema Mkuu wa Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
Mwilapwa aliongeza kuwa nia ya Serikali ni kuwaepusha wanafunzi katika misongamano ili kujikinga na virusi vya corona na si kudhoofisha katika masomo wananfunzi ndio maana wameamua kuchukua uamuzi mgumu .
Mwilapwa amesisitiza kuwa kwa Yeyote aliyeyefungua kijiwe kwaajili ya kuwafundisha vijana kama tution afunge mara moja kwani kitakachofuata baada ya tangazo hili ni hatua za kisheria .
Nia ya Serikali ya kuwaruhusu wanafunzi wote kurudi majumbani ni kuwatoa katika mikusanyiko ambayo inaweza sababisha maambukizi ya virusi vya corona kuenea kwa haraka ambavyo vimekuwa vikisambaa katika maeneo mbalimbali nchini .
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.