Mkuu wa Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa alipokea Mwenge wa Uhuru 2021 mara baada ya Kuwasili Mkoani Tanga Ukitokea Visiwani Zanzibar ambapo kwa Wilaya ya Tanga ulikimbizwa katika Tarafa Nne na kupitia miradi 10 yenye thamani ya zaidi ya Bil.3.
Akisoma risala kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2021 Josephine Mwambashi mara baada ya kupokea Mwenge wa Uhuru katika Uwanja wa Ndege Mwilapwa alisema kuwa “katika Miradi 10 iliyokuwepo Miradi Miwili ilifunguliwa, miwili iliwekwa mawe ya Msingi,Mitano Ilikaguliwa na mingine ni ile iliyotekelezwa kupitia mapato ya ndani kama ilivyoainishwa na serikali kuhusu asilimia 10% ya mapato ya Ndani”.
Kituo cha Sayansi na Maabara ya tehama ni moja ya miradi iliyozinduliwa na kuwekewa jiwe la Msingi ambapo kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru akasisitiza juu ya suala la umuhimu wa matumizi sahihi ya Tehama kama “Ujumbe wa Mbio za mwenge wa uhuru kitaifa 2021 iliyosema Tehama ni msingi wa taifa endelevu itumike kwa Usahihi na Uwajibikaji”.
Naye Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Josephine Mwambashi akatoa rai kwa wananchi kutumia vizuri Teknolojia kwani endapo utatumia kwa matumizi ambayo si mazuri zipo sheria.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.