Mwenge wa Uhuru kwa Mwaka 2017 umepitia jumla ya Miradi Saba (7) yenye thamani ya Jumla ya Tsh. 15,072,295,848.90. Thamani hii imepatikana kwa fedha kutoka Serikali Kuu, Halmashauri na Nguvu za Wananchi
1: UENDELEZAJI WA SHAMBA LA MITI MLENI
Eneo hili lenye ukubwa wa Ekari 161 lilitwaaliwa na Halmashauri ya Jiji la Tanga miaka ya 70 kwa lengo la kuhamasisha utunzaji wa Mazingira kutokana na hali ya jangwa inayolikabili eneo hili. Kwa kipindi chote shamba hili lilipandwa miti ya Mijohoro na sehemu kubwa iliachwa vichaka vya asili. Mnamo mwaka 2009 Halmashauri iliamua kuliendeleza shamba kwa kupanda miti ya Tiki. Ambapo hadi sasa ekari 41.5 zimepandwa miti hiyo yenye jumla ya miti 40,000.
Faida za mradi huu ni kama zifuatazo:-
Thamani ya mradi ni Tsh. 1,062,600,000.00
2: KILIMO CHA MBOGAMBOGA NA MATUNDA - KIOMONI
Shamba lina ukubwa hekta 27.7. Ekari 1 imelimwa kilimo cha kisasa cha umwagiliaji kwa njia ya matone na Hekta 26 zimelimwa kilimo cha kawaida na zinaendelezwa.
Lengo la Mradi huu ni;-
Faida za Mradi ni kama ifuatavyo:-
Matarajio ya baadae ni kutanua mradi wetu kwa eneo lilobakia ili kuweza kulima kisasa katika eneo lote na kuongeza tija ili kuweza kutoa malighafi za viwanda hasa vya matunda na usindikaji wa mbogamboga ili kupata soko la ndani na nje.
Thamani ya mradi ni Tsh. 30,120,000.00
3: UJENZI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU (MADARASA, OFISI NA VYOO) SHULE YA MSINGI BOMBO
Shule ya Msingi Bombo ni miongoni mwa Shule tatu za Umma zilizopo ndani ya kata ya Central. Shule ina jumla ya wanafunzi 1,036 wavulana 564 wasichana 472. Kuna walimu 18 wanaume 2 wanawake 16. Shule hii imejengwa upya baada ya jengo la awali kusitishwa kutumika kutokana na uchakavu.
Jengo hilo la zamani lilijengwa mnamo mwaka 1902 na kuanza kutumika kama shule ya Awali mwaka 1945, na baadae kuwa shule ya Msingi. Jengo hilo lilikuwa la ghorofa moja, ndani yake lilikuwa na huduma zote muhimu za shule.
Wanafunzi wote walihama kwa muda na kushirikiana vyumba vya madarasa katika Majengo ya Shule ya Msingi Mkwakwani baada ya jengo hilo kutofaa kutumika tena na hivyo kusababisha msongamano mkubwa katika Shule ya Msingi Mkwakwani.
Halmashauri ilianza ujenzi wa majengo mbadala mwezi Septemba 2016, kwa kujenga vyumba sita (6) vya madarasa kwa mapato yake ya ndani. Na vilevile ujenzi unaendelea wa vyumba vitano (5) vya madarasa, jengo la utawala na vyoo kwa fedha za Serikali kuu kupitia mpango wa Lipa Kulingana na Matokeo (Payment for Results – P4R).
Faida zitakazopatikana kutokana na mradi huu ni:-
Kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia.
Kupunguza msongamano katika jengo la shule ya msingi Mkwakwani
Thamani ya mradi ni Tsh. 408,707,710.00
4: DUKA LA DAWA LA JAMII
Lengo kuu la Maduka haya ya dawa ni kuimarisha huduma bora za afya kwa jamii na kuwezesha upatikanaji wa dawa, vitendanishi na vifaa tiba karibu zaidi na Wananchi, kwa muda wote, ubora unaokubalika na kwa bei nafuu.
Huduma zinazotolewa ni upatikanaji wa dawa zote zilizopo katika orodha ya dawa za Bohari Kuu ya Dawa (MSD) na zisizo katika orodha (Generic and Brands Medicines), huduma ya dawa kwa wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), dawa kwa jamii, Dawa kwa Taasisi za serikali na binafsi kwa waliosajiliwa kwa mujibu wa sheria.
Faida za mradi huu ni kama ifuatavyo:-
Kurahisisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa wananchi kwa bei nafuu, kupunguza urasimu wa ununuzi wa dawa, vitendanishi na vifaa tiba katika ngazi ya Vituo vya kutolea Huduma za Afya na Kuwezesha upatikanaji wa dawa, vitendanishi na vifa tiba katika Vituo vya kutolea Huduma za Afya kwa 100%.
Kusogeza huduma ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).Vilevile ni Kivutio kikuu kwa Wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii/TIKA kutokana na kuwa na uhakika wa uwepo wa dawa, vitendanishi na vifaa tiba vituoni.
Kuongeza mapato ya ndani ya Halmashauri
Kuviondoa/kupunguza kabisa Vituo vya Umma kununua dawa, vitendanishi na vifaa tiba kwa washitiri (Prime vendors).
Duka la dawa la jamii ni jibu sahihi la kumaliza tatizo la muda mrefu la upungufu wa dawa katika Vituo vya kutolea Huduma za Afya vya Umma hivyo litaboresha sana upatikanaji wa dawa, vitendanishi na vifaa tiba kwa wananchi wa Jiji la Tanga na mkoa kwa ujumla. Kwa heshima kubwa tunakuomba utufungulie mradi wa duka letu.
Thamani ya mradi ni Tsh. 451,000,000.00
5: UKARABATI WA JENGO LA KITUO CHA TANGA TELEVISHENI
Kituo cha Tanga Television (TaTV) kilianzishwa mwezi Mei 2004 katika jengo dogo lililopo eneo la Fire kikiwa kinatumia mfumo wa analogia, baada ya Vituo vya Televisheni vilivyokuwa vikionekana Tanga kwa wakati huo kutokidhi mahitaji muhimu ya wakazi wa Tanga yahusuyo maisha yao ya kila siku kama vile elimu, utamaduni na siasa. Mnamo mwaka 2014 TaTV ilibadilisha mfumo wa utangazaji kutoka analogia kwenda mfumo wa digitali ambao ulihitaji kubadilisha vifaa mbalimbali na jengo ili viendane na mfumo huo.
Katika kuboresha huduma za Kituo, Halmashauri imekarabati moja ya jengo hili lililopo eneo la Tangamano ili kuipatia TaTV Ofisi na Studio zinazoendana na mahitaji ya utendaji kazi wake. Kabla ya hapo jengo hili lilikuwa likitumika kama Ofisi ya Mtendaji Kata. Kwa sasa kituo chetu kinaonekana Mkoani Tanga na Kisiwani Pemba kupitia king’amuzi cha StarTimes, pamoja na Cable TV za Jijini Tanga.
Faida za Mradi huu ni kama ifuatavyo:-
Kuifahamisha jamii ya wakazi wa Tanga juu ya matukio ya kiserikali na kijamii yanayotokea ndani na nje ya Wilaya na Mkoa wetu Kitaifa na Kimataifa.
Kutoa elimu juu ya mambo mbalimbali, mfano Afya ya Jamii, ujasiliamali, n.k
Kuonyesha shughuli mbalimbali zinazofanywa na Halmashauri, na Baraza la madiwani (ikiwemo vikao vya Baraza la madiwani)
Kuinua vipaji vya wasanii wa Tanga kwa kuzitangaza kazi zao.
Kutoa fursa kwa watazamaji kuwasiliana na watendaji wa sekta mbalimbali moja kwa moja kupitia vipindi vya mahojiano (live programme)
Kutoa burudani kupitia muziki, filamu na michezo mbalimbali inayoonyeshwa na kituo.
Kupitia Kituo hiki, wakazi wa Tanga na Taifa kwa ujumla watapata elimu na habari juu ya fursa za ajira katika uwekezaji mkubwa unaokuja Tanga, uelewa wa kutosha juu ya Tanzania ya Viwanda, na umuhimu wa kutunza na kuimarisha afya zao.
TaTV inamatarajio ya kupanua huduma zake ionekane kitaifa.
Thamani ya mradi ni Tsh. 136,986,799.00
6: eneo maalum lililotengwa kwa ajili ya viwanda pongwe (PONGWE INDUSTRIAL PARK)
Lengo la mradi huu ni kutengeneza mazingira mazuri ya uwekezaji wa viwanda ili kuongeza ajira na kipato kwa Mwananchi mmoja mmoja, Halmashauri na Taifa kwa ujumla.
Mradi huu ulianza tarehe 03/01/2017 na kukamilika tarehe 10/08/2017 ikiwa ni sehemu ya mradi mkubwa wa upimaji wa maeneo mbalimbali ndani ya Halmashauri ya Jiji la Tanga ambapo lengo ni kukamilisha upimaji na viwanja 4,707 kwa awamu ya kwanza.
Mradi huu una jumla ya viwanja 101 kati ya hivyo vya viwanda 98 ambavyo vina ukubwa wa ekari 2.5 hadi ekari 3 kwa kila kiwanja, vituo vya mafuta ni viwili (2) na kiwanja kimoja ni kwa ajili ya maegesho ya malori.
Sambamba na mradi huu ni upimaji mwingine unaoendelea wa eneo la viwanda la Kiomoni ambapo itaitwa Kiomoni Industrial Park yenye jumla ya viwanja 182 vyenye ukubwa wa kati ya ekari 6 hadi 8.
Manufaa ya mradi huu ni pamoja na:-
Uwepo wa Ardhi iliyopangwa na kupimwa kuvutia wawekezaji kwenye sekta ya viwanda.
Kuzalisha ajira nyingi baada ya viwanda kukamilika.
Halmashauri itajipatia Tshs. 10,281,857,000.90 kutokana na mauzo ya viwanja.
Serikali kuu itapata kodi mbalimbali kama kodi ya Ardhi n.k
Thamani ya mradi ni Tsh. 10,281,857,000.90
7: UJENZI WA BARABARA YA NGUVUMALI
ujenzi wa Barabara ya Nguvumali kiwango cha Lami yenye urefu wa kilomita 1.6, barabara hii ni sehemu ya miradi miwili inayofadhiliwa na Benki ya Dunia Katika Jiji la Tanga yenye urefu wa kilomita 2.7 ambayo ni barabara ya Jamatcan kilomita 1.1 na ya Nguvumali
Hapo awali barabara hii ilikuwa ya kiwango cha changarawe na ilikuwa haiko katika hali ya kuridhisha na hivyo kusababisha usumbufu kwa Wakazi wa eneo hilo hasa katika kipindi cha majira ya mvua.
Mradi huu ulianza tarehe 01/07/2016 kupitia Bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/2017 chini ya Mradi wa uendelezaji Miji (TSCP) ambao unafadhiliwa na Benki ya Dunia, chini ya Serikali kuu .Mradi unatekelezwa na mkandarasi wa Kampuni ya M/S Hari Sigh&Son,s Ltd, Moshi Tanzania.
Mradi huu unasimamiwa kwa pamoja kati ya Halmashauri ya Jiji Tanga na Mhandisi Mshauri Kampuni ya UWP Consulting (T) Ltd, chini ya uangalizi wa ofisi ya Rais TAMISEMI.
Lengo la mradi huu ni kuboresha miundombinu ya barabara ndani ya Jiji la Tanga na hivyo kurahisisha mawasiliano kutoka eneo hili kwenda maeneo ya mengine ya Mji na hivyo kuwapunguzia usumbufu wa usafiri wakazi wa eneo hili kwani itaweza kutumika wakati wote katika kipindi cha mwaka.
Faida za Mradi huu ni kama ifuatavyo:-
Kurahisisha mawasiliano kwa wakazi wa eneo hili wanaotumia barabara hii.
Kupendezesha mji, kwa uwepo wa barabara nzuri
Kuboresha usalama na mazingira ya mji kwa uwepo wa taa za barabarani
Thamani ya Mradi ni Tsh. 2,701,024,339.00
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.