Jumla ya vyumba vya madarasa 12,000 vya shule za awali na msingi za Serikali hapa nchini, vinatarajiwa kujengwa kwa kupindi cha miaka mitano kupitia mradi wa BOOST katika maeneo yenye upungufu au msongamano wa wanafunzi.
Akifungua mafunzo elekezi ya utekelezaji wa mradi huo kwa wajumbe wa timu za utekelezaji za Mikoa na Halmashauri kutoka Tanga na Kilimanjaro, Afisa Elimu Mkoa wa Tanga Bi. Newaho Mkisi amesema thamani ya mradi huo ni Tsh. Triilioni 1.15 kwa nchi nzima, fedha hizo zikitolewa na Serikali kwa kushirikiana na Bank ya Dunia.
Amesema utekelezaji wa mradi utakuwa wa lipa kwa matokeo, hivyo timu za utekelezaji zitapaswa kufanya kazi kwa matokeo ili kuwezesha mradi kuendelea na kusaidi kuondosha changamoto zilizopo katika elimu ya awali na msingi.
Katika kipindi cha miaka mitano ya utekelezaji wake, Mradi wa Boost unatarajiwa kujenga vyumba vya madarasa 12,000, kutoa vifaa vya tehama kwa shule za msingi na vituo vya mafunzo kwa walimu 8,000, mpango wa shule salama 6,000, kuongeza uandikishaji wa elimu ya awali kufikia asilimia 85 ya uandikishaji.
Mafunzo hayo ya siku mbili yanafanyika katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe yakiwakutanisha wataalamu 231 kutoka Halmashauri 11 za Mkoa wa Tanga na Halmashauri 7 za Mkoa wa Kilimanjaro katika sekta za elimu, mipango, uhandisi, manunuzi, na zingine katika Halmashauri.
Mradi wa Boost unatarajiwa kuboresha mazingira ya ujifunzaji na ufundishaji, ujuzi na ubora wa walimu katika ufundishaji, pamoja na kuimarisha upatikanaji wa rasilimali za utoaji huduma za elimu ngazi ya Halmashauri.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.