Mkuu wa wilaya ya tanga thobias mwilapwa amesema amesikitishwa na kushangazwa na vitendo vya baadhi ya watu ambao wameanza tabia ya kuiba koki za ndoo zinazowekwa kwa lengo la kujikinga na maambukizi dhidi ya ugonjwa wa corona .
Mwilapwa amesema kuwa alipata taarifa za kufanyika kwa wizi huo katika soko la Ngamiani ambapo kuna baadhi ya watu wanafanya uharifu huo nyakati za usiku .
Akizungumza na tanga televisheni Mwilapwa alisema suala la kujikinga na ugonjwa wa Corona ni la Wananchi wote na si Serikali peke yake hivyo waache tabia hiyo kwani itasababisha kuongezeka kwa maambukizi ya ugonjwa wa corona nchini .
“ Kama kiongozi nimeshituka sana baada ya afisa mtendaji wa kata ya Ngamiani kuniambia ndoo tulizonunua kwaajili ya kupambana na ugonjwa wa corona zimechomolewa koki na watu wasiojulikana nyakati za usiku hii inamaana sisi tunapambana ili kuweza kudhibiti ugonjwa huu wengine wanania mbaya na sisi tukiwabaini hawa hatua kali zitachukuliwa “Alisema Thobias Mwilapwa
Mwilapwa aliongeza kwa kuwataka wananchi kuzingatia kanuni na taratibu wanazopewa na wataalamu wa afya kwa kupunguza mikusanyiko yakiweo matamasha,mazoezi mbalimbali kama ya ngumi ,uchezaji wa drafti na vitu ambavyo husababisha mikusanyiko hiyo .
Ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na Virusi vya Covid 19 umesambaa katika maeneo mbalimbali Duniani ambapo mpaka sasa Tanzania ina jumla ya wagonjwa 88 wenye maambukizi hayo huku waliopona ni 11 na 3.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.