Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mheshimiwa Omari Mgumba, jumamosi ya Augosti 20, 2022, amewaongoza Wakazi wa mkoa wa Tanga katika Matembezi ya amani kwa ajili ya kuhamasisha ushiriki wa zoezi la Sensa ya Watu na Makazi litakalofanyika siku ya Jumanne ya tarehe 23 Augosti 2022.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa matembezi hayo, Mgumba ameeleza umuhimu wa sensa katika kupata takwimu sahihi zitakazoisaidia serikali kupanga mipango ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa amesema wao kama Wilaya wanaendesha zoezi la hamasa la mtaa kwa mtaa katika Jiji la Tanga liitwalo "mtaa kwa mtaa Tanga na sensa 2022" linalowahusisha vijana takribani 40 wakipita kila mtaa lengo likiwa ni kutoa elimu ya sensa kupitia burudani.
Nao Baadhi ya watumishi wa serikali waliohudhuria matembezi hayo, wamempongeza Mama Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuifanya siku ya sensa kuwa ya mapumziko ili waweze kushiriki kikamilifu katika zoezi la sensa kwa kutoa taarifa sahihi wao wenyewe tofauti na kuacha kwa watoto au jirani.
Katika zoezi hilo pia wananchi wamepata nafasi ya kushiriki zoezi la upimaji wa afya lililoendeshwa na Kitengo cha Lishe, Idara ya Afya ya Halmashauri ili kutambua hali zao pamoja na kupata elimu ya kujiepusha na magonjwa yasiyoambukizwa.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.