Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Bw. Said Majaliwa, amefanya kikao na Mafundi Ujenzi wanaofanya kazi na Halmashauri, chenye lengo la kusikiliza kero na changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikiwakabili mafundi hao, katika utekelezaji wa miradi ya Halmashauri.
Akizungumza katika kikao hicho, kilichofanyika kwenye ukumbi wa ofisi za Makao Makuu ya Halmashauri, Mkurugenzi Majaliwa amewaahidi mafundi hao kuzifanyia kazi kero na changamoto zote walizozitoa, ili miradi iishe kwa wakati.
Aidha Majaliwa amewataka mafundi wanaodai malipo kwa kazi ambazo tayari walishaandaa certificate za madai, kufika ofisini kwake ili kuona namna ya kuwalipa madeni yao.
Amesema atahakikisha anatatua changamoto zao lakini amewaomba mafundi kufanya kazi na kumaliza mradi katika muda uliopangwa.
Amewakumbusha Mafundi hao kuhakikisha wanajisajili katika Mfumo wa NeST na ametoa wataalamu wa Ofisi ya manunuzi kuwasaidia jinsi ya kujisajili katika mfumo. Msaada huo utakuwa wa siku saba
Pia Mkurugenzi Majaliwa amewataka wahandisi kuhakikisha wanasimamia miradi na kuwaacha mafundi walioanza mradi husika kuendelea na ujenzi wa mradi mpaka utakapokamilika.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.