Mamlaka ya usimamizi wa bandari Tanzania kwa niaba ya serikali imeanza kuboresha miundo mbinu ya bandari ya Tanga kwa kuleta vifaa vipya vya kisasa ili kuboresha kasi ya utoaji huduma wa bandari hiyo.
Akizungumza leo na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa bandari hiyo mkuu wa bandari ya Tanga Percivar Salama amesema mamlaka ya usimamizi wa bandari Tanzania imefanya kazi kubwa ya kuboresha miundo mbinu ya bandari ya Tanga kwa kuwapatia vifaa vipya na vya kisasa ikiwa ni pamoja na boti ya ulinzi.
Aidha mkuu wa bandari ya Tanga ameeleza kuwa boti hiyo itasaidia kuimarisha ulinzi kwa kuwadhibiti watu ambao huingiza bidhaa nchini kinyume cha sheria na kuwataka wafanyabiashara wote hapa nchini wanaotumia bandari za Tanga kutumia bandari ambazo zimeainishwa kisheria ikiwa ni bandari ya Tanga na Pangani.
Hata hivyo bandari ya Tanga ni bandari pekee Afrika inayoweza kuhudumia nchi saba kwa kutumia mpaka mmoja ambapo nchi hizo ni Malawi, Zambia, Demokrasia ya congo, Burundi, Rwanda, Uganda na nchi jirani ya Kenya.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.