Mkurugenzi wa Jiji la Tanga, Ndg. Said Majaliwa, amekagua utekelezaji wa mradi wa uboreshaji upatikanaji wa fursa sawa katika ujifunzaji bora wa Elimu ya Awali na Msingi (BOOST), uliotekelezwa katika Jiji la Tanga, kwa mwaka wa fedha 2022/2023, ambapo kiasi cha zaidi ya shilling million 940 zilitumika kwa ujenzi wa shule mpya moja, vyumba vya madarasa 12, Madarasa 2 ya mfano ya elimu ya awali na matundu 15 ya vyoo.
Bw. Majaliwa amewataka wasimamizi wa miradi hiyo kuhakikisha wanakamilisha maeneo ambayo bado, ili kuwezesha majengo hayo kutumika kama yalivyokusudiwa.
Mkurugenzi Majaliwa amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha nyingi katika Jiji la Tanga za ujenzi wa miundombinu ya elimu kupitia mradi wa BOOST, na hivyo kuwezesha wanafunzi kukaa vizuri darasani, jambo linalowafanya kufurahia shule na kupata usikivu mzuri wa masomo.
Shule za Msingi za Jiji la Tanga zilizo nufaika na mradi kwa mwaka wa fedha 2022/2023, ni pamoja na ujenzi wa shule mpya Jaje, Madarasa mawili ya elimu ya awali Mapojoni, vyumba vitatu kwa kila shule za Bombo, Mabawa, Mapambano na Msala. Ambapo ujenzi wa majengo hayo umejumlisha na ununuzi wa madawati, meza na kiti cha Mwalimu kwa kila darasa.
Wakati Jiji la Tanga likiwa limepokea shilling million 940,900,000.00, jumla ya fedha ya BOOST kwa mwaka wa fedha 2022/2023 iliyotolewa kwa Mkoa wa Tanga ni shilling Billion 11,422,000,000.00 ambapo zilipangwa kujenga shule mpya za Msingi 15, sambamba na vyumba vya madarasa 140 pamoja na miundombinu mingine.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.