Rais mstaafu wa awamu ya nne Mhe .Jakaya Mrisho Kikwete amepongezaTaasisi ya Maawal Islamic kwa mchango wao wa kusaidia sekta ya elimu mkoani tanga hasa kwa watoto wa kike kwa kuwajengea bweni ili kuweza kuwatengenezea mazingira mazuri ya kujifunza
Ameyasema hayo siku ya jumapili alipokuwa akiweka jiwe la msingi la uzinduzi wa bweni kwa ajili ya watoto wa kike katika shule ya sekondari Maawal Islamic iliyopo jijini hapa
Ameongeza kuwa Lengo kubwa la kuanzisha Taasisi hiyo ni kufundisha dini ya kiislamu katika jiji hili na jambo jingine na kufanya mambo muhimu yanayohusu kijamii na kupinga dhana ya kusema waislamu hawajali elimu ya mtoto wa kike.
“Hili ni jambo la furaha kwa sababu kumekuwepo na dhana kwamba sisi waislamu hatujali elimu ya mtoto wa kike leo watoto wa kike wemgi wanasoma na walimu wetu wanasaidia kututengenezea mawaziri wa baadae”Amesema mhe kikwete.
Mkuu wa mkoa wa tanga Martine Shigela amesema Mkoa wa Tanga ni moja kati ya Mikoa ambao umepata mafanikio makubwa katika Sekta mbalimbali ikiwemo Ufya ,ujenzi na katika sekta ya Elimu na mambo mbalimbali .
Amesema mafanikio yote hayo ni matokeo ya kazi nzuri anayoifanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkr John Pombe Magufuri pamoja na msingi mzuri aliouanzia Rais wa awamu ya nne Mhe Jakaya Mrisho Kikwete .
“sisi kama wasaidizi wa rais hatuna budi kuendeleza haya yote uliyoyaanzisha lakini pia tunashukuru mafanikio katika sekta ya elimu kazi nzuri uliyoianzisha ya ujenzi wa shule ya sekondari kila kata lakini awamu ya tano inatekeleza na kuhakikisha inatoa elimu bure “Amesema Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela
Kiongozi wa taasisi hiyo shekh Mohamed Hariri ambae ni Mkuu wa Taasisi hiyo ya Maawal Islamic amesema kituo hicho kitawasaidia wanafunzi hao kuepuka mambo mbalimbali ambayo ni mabaya yanayoweza kujitokeza juu yao
Taasisi ya Maawal Islamic ni moja kati ya Taasisi ambazo zinatoa mafunzo kwa wanafunzi wa kike na wakiume kikiwa na lengo la kutoa mafunzo ya dini ya kiislamu pamoja na mafunzo ya kusaidia jamii kinachopatikana Jijini Tanga
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.