Na: Winfrida Paul
Timu ya wataalam washauri kutoka Jumuiya ya Ulaya (EU), chini ya mradi wa Green and Smart City SASA, wamefika katika Jiji la Tanga kwa ajili ya kuendelea na hatua za matayarisho ya ujenzi wa soko la Mgandini, na kutembelea eneo ambalo wafanyabiashara watahamia kwa muda ili kupisha ujenzi wa soko hilo.
Diwani wa Kata ya Mwanzange Mhe. Bakari Ally Mtavya, amesema soko hilo linakadiriwa kujengwa kwa muda wa miezi 18 hadi 24 na litakapokamilika litakuwa faraja kubwa kwa wafanyabiashara na wakazi wa Tanga kwa ujumla kwani soko hilo linategemewa na wakazi wa jiji hilo pamoja na nchi za jirani.
Kwa upande wake mratibu msimamizi wa mradi huo Kizito Nkwabi amesema mradi huo umekuja kuweka vizuri mifumo ya chakula katika jiji la Tanga ikiwa ni pamoja na ujenzi wa soko hilo.
Aidha Kizito amesema pia wataalamu hao wamekuja kufanya upembuzi yakinifu wa mradi huo na kukagua eneo lililopendekezwa kwa ajili ya wafanyabiashara kuhamia.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.