Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga, Mustapha Seleboss amakea tabia ya watu wazima kuwarubuni watoto wadogo wa kike na hatimae kuwafanyia vitendo visivyoendana na maadaili, Amekemia hayo leo akiwa kwenye sherehe za uzinduzi wa bweni jipya la watoto wa kike kwenye kituo cha GOODWILL AND WOMEN FOUNDATION Mtaaa wa Mwakidila, Jijini Tanga.
“Sisi kama wazazi, walezi ni lazima tukemee watu wazima wasiokuwa na akili timamu kuwafanya watoto wadogo hawa kuwa kama wake zao”, alisema Mstahiki Meya
Akiendelea kukemea tabia hiyo, alisema kuwa Kituo hiki kiwe kama sehemu ya kuwalea na kuwalinda watoto dhidi ya watu wazima wenye matamanio ya nafsi na ambao hawana akili za kiutu uzima ambao hawawatakii mema watoto kwa kuwarubuni kwa hela au vitu vidogovidogo, na kuwafanya watoto hao kuwa kama wake zao.
Akiaongea kwa niaba ya wenzake, mmoja kati ya watoto wanaishi kwenye kituo hicho, aliwashukuru wote wanaowasaidia na kwa kuwa wanatoa kwa nia njema Mungu atawalipa. Aliwaomba wanaotaka kutoa wanakaribishwa na haoni sababu ya kutoa na kujitangaza kwani kama wanatoa kwa nia njema Mungu anaiona na atawalipa. Akiendelea kuongea kwa uchungu akionesha masikitiko yake kwa watu ambao wanajinufaisha kwa uwepo wao kama watoto yatima. “Kuna watu wanakula, wanavaa, anakuwa na magari, ana viwanda kwa ajili ya neno yatima, neno yatima kwake ndio kipato. Anafanya unyonge wetu sisi, udhaifu wetu sisi, yeye kwake ndio ashibe, ale na avae” alisema mtoto huyo aliyejulikana kwa jina la Maze Fred.
Taasis ya GOODWILL AND WOMEN FOUNDATION ilianzishwa tarehe 24 mwezi machi 2016. Imesajili kwa ajili ya kuhudumia watoto yatima, wazee, wajane, walemavu na wagonjwa walioshindwa gharama za matibabu. Taasis inahudumia watoto 288, ndani ya kituo kuna watoto 25, ikiwa wengine wapo wanlelewa na walezi wao lakini taasis inawahudumia hukohuko walipo.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.