Mkurugenzi wa Jiji la Tanga, Dkt. Sipora Liana, leo Mei Mosi, 2023, amewaongoza Watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, yaliyofanyika katika Uwanja wa michezo wa Mkwakwani Jijini Tanga.
sherehe hizo zilizofanyika kimkoa katika Jiji la Tanga, zilihutubiwa na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mhe. Hashim Mgandilwa ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Waziri Kindamba, na kuhudhuriwa na wafanyakazi kutoka wilaya za Mkoa wa Tanga, ambapo zawadi mbalimbali zilitolewa kwa wafanyakazi hodari kutoka vyama vya wafanyakazi kuwakilisha taasisi wanazofanyia kazi.
Miongoni mwa taasisi zilizotoa zawadi kwa wafanyakazi hodari ni Jiji la Tanga, ambapo watumishi hodari kwa mwaka huu wamepata zawadi ya fedha na vyeti.
Independent Avenue
Sanduku la Posta : P.O.BOX 178, Tanga
Simu ya Mezani: 027 2643068
Simu ya Mkononi:
Baruapepe: info@tangacc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Jiji la Tanga . Haki Zote Zimehifadhiwa.